SOMO LA FIQHI
Yanayoharamishwa kwa mwenye janaba
1. KUSWALI:
Kwa neno lake Mwenyazi Mungu Aliyetukuka:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا} النساء:43}
[Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge] [Al-Nisaa 43]
2. KUTUFU NYUMBA TUKUFU (Alkaba):
Kwa neno lake Mtume ﷺ:
[الطواف صلاة إلا أن الله تعالى أحل فيه الكلام؛ فمن تكلم فلا يتكلم إلا بخير]
[Kutufu Alkaba ni kama kuswali isipokuwa Mwenyezi Mungu amehalalisha kuzungumza,basi atakae zungumza asizungumze ila kwa kheri] [Imepokewa na Nasai.].
3. KUGUSA MSAHAFU:
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ} الواقعة:79
[Hawaigusi isipokuwa waliotwahirishwa] [56: 9].
Na neno la Mtume ﷺ :
[لا يمس القرآن إلا طاهر] رواه مالك في الموطأ
[Haugusi Msahafu isipokuwa aliye Twahara] [Imeipokewa na Malik katika Muwatta’.]
4. KUSOMA QUR’ANI TUKUFU:
Imepokelewa kutoka kwa Sayyidna Ali Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
[كان النبي صلى الله عليه وسلم يقرئنا القرآن ما لم يكن جبنا] رواه أحمد في المسند
[Alikuwa Mtume ﷺ Akitusomea Qur’ani isipokuwa akiwa na janaba] [ Imepokewa na Ahmad katika Musnad].
5. KUKAA MSIKITINI ISIPOKUWA KWA MPITA NJIA:
Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا}
[Enyi mlioamini! Msikaribie Swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo sema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge]. [ Al-Nisaa 43]