0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HALI AMBAZO HUSUNIWA MTU KUOGA

SOMO LA FIQHI

Kuoga kunakopendekezwa

1. KUOGA KWA AJILI YA SWALA YA IJUMAA

Kwa kauli ya Mtume ﷺ:

[من توضأ، فبها ونعمت، ومن تغسل فالغسل أفضل]    رواه أبوداود

[Mwenye kutawadha kwa ajili ya kwenda Ijumaa, hilo ni jambo zuri, na mwenye kuoga, basi kuoga ni bora]    [Imepokewa na Abu Daud.]

2. KUOGA WAKATI WA KUHIRIMIA KWA AJILI YA UMRA NA HIJA.

Imepokewa kutoka kwa Zaid bin Thabit kwamba yeye alimuona Mtume ﷺ:

[تَجَرَّدَ لإِهلالِهِ وَاغتَسَلَ]   رواه الترمذي

[Akijiondoa na nguo za kawaida kwa ibada ya Hija na akaoga]   [Imepokewa na Tirmidhi]

3. KUOGA BAADA YA KUOSHA MAITI.

[مَن غَسَّلَ مَيتًا فَلْيَغتَسِلْ]    رواه أحمد والترمذي

Kwa neno la Mtume ﷺ: [Mwenye kuosha maiti aoge]     [Imepokewa na Ahmad na Attirmidhiy.]

4. KUOGA BAADA YA KILA TENDO LA NDOA.

Imepokewa na Abu Rafi’i radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume :

طَافَ ذَاتَ يَوْمٍ عَلَى نِسَائِهِ يَغْتَسِلُ عِنْدَ هَذِهِ وَعِنْدَ هَذِهِ ، قَالَ قُلْتُ : لَهُ يَا رَسُولَ اللَّهِ أَلَا تَجْعَلُهُ غُسْلًا وَاحِدًا قَالَ :  هَذَا أَزْكَى وَأَطْيَبُ وَأَطْهَرُ

[Siku moja aliwapitia wake zake, na alikuwa akioga baada ya kumaliza kwa huyu na kwa yule. Mpokeaji asema: (Nikamwambia”Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! usiuoge mara moja? Akasema ﷺ  [Hili ni safi zaidi, bora zaidi na twahara zaidi]         [Imepokewa na Abu Daud.]

MAKATAZO

1- kuchelewesha kuoga janaba mpaka utoke wakati wa Swala.

2- kwa mwanamke aliyetwahirika na hedhi kuacha Swala ya wajibu. Na lau atwahirika kabla ya kutoka wakati wa adhuhuri kwa kadiri ya rakaa moja, basi itampasa aoge na aswali adhuhuri. Mtume ﷺ amesema:

من أدرك من الصبح ركعة قبل أن تطلع الشمس فقد أدرك الصبح ومن أدرك ركعة من العصر قبل أن تغرب الشمس فقد أدرك العصر

[Mwenye kuwahi rakaa moja ya asubuhu kabla ya kuchomoza jua, basi amewahi Swala ya asubuhi. Na mwenye kuwahi rakaa moja ya alasiri kabla ya jua kuzama, basi amewahi Swala ya alasiri]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.