0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YANAYOFAA KUFANYA IKIWA MTU AMEFUNGA

MAMBO YANAYOFAA KUFANYA IKIWA MTU AMEFUNGA

1. Kuoga, na kukaa mahali penye maji ili kupata baridi.

2. Kumeza mate na makohozi.

3. Kuonja chakula ili kujua kiwango cha sukari au chumvi yake kwa kutumia ulimi peke yake, kwa sharti asiingize chochote katika chakula hicho hadi kwenye koo.

4. Kunusa harufu ya manukato na visafisha hewa.

FAIDA

Matumizi ya mswaki kwa mtu aliyefunga
Yaruhusiwa kutumia mswaki kwa mtu aliyefunga wakati wowote ule, sawasawa iwe ni kabla ya kuzama kwa jua kwa kuingia jioni au baada ya hapo, na vilevile uwe mswaki wenyewe uko majimaji au mkavu, lakini anatahadharishwa aliyefunga ikiwa mswaki anaotumia uko majimaji kusije kukaingia chochote kooni wakati anapiga mswaki; kwa sababu kuingia kwa kitu kooni kunaharibu saumu yake.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.