0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO AMBAYO HUMZUIYA MTU KURITHI

SOMO LA MIRATHI

Mambo ambayo huzuiya mtu kurithi

1. Mtumwa harithi wala harithiwi, na iwapo amerithi basi vyote alivyo vimiliki ni mali ya Bwana wake.

2. Muuwaji; mtu alieuwa kwa ajili ya  kurithi, basi hatopata kitu chochote katika mali ya yule anae mrithi, kwa mujibu wa maneno ya Mtume Muhammad ﷺ

[لَا يَرِثُ الْقَاتِلُ شَيْئًا]    رواه أبوداود

[Hatorithi muuaji mali kitu chochote ].   [Imepokelewa na Abuu Dawuud]

3. Kukhitilafiana kwa dini nayo ni: muislamu na asiye kuwa muislamu hata kama ni ndugu, haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume ﷺ

[لا يرث المسلم الكافر ولا الكافر المسلم]

[Hamrithi muislamu kafiri wala kafiri hamrithi muislamu].     [Imepokelewa na Bukhari]

4. Mtoto aliezaliwa nje ya ndoa (isipokuwa ikiwa maiti akiacha wasia).

Chanzo:UADILIFU WA MIRATHI NDANI YA UISLAMU

Manswab Mahsen Abdul RahmaAl-Ridai Al- Jufry Uk 4

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.