SOMO LA MIRATHI
Mambo ambayo huzuiya mtu kurithi
1. Mtumwa harithi wala harithiwi, na iwapo amerithi basi vyote alivyo vimiliki ni mali ya Bwana wake.
2. Muuwaji; mtu alieuwa kwa ajili ya kurithi, basi hatopata kitu chochote katika mali ya yule anae mrithi, kwa mujibu wa maneno ya Mtume Muhammad ﷺ
[لَا يَرِثُ الْقَاتِلُ شَيْئًا] رواه أبوداود
[Hatorithi muuaji mali kitu chochote ]. [Imepokelewa na Abuu Dawuud]
3. Kukhitilafiana kwa dini nayo ni: muislamu na asiye kuwa muislamu hata kama ni ndugu, haya ni kwa mujibu wa maneno ya Mtume ﷺ
[لا يرث المسلم الكافر ولا الكافر المسلم]
[Hamrithi muislamu kafiri wala kafiri hamrithi muislamu]. [Imepokelewa na Bukhari]
4. Mtoto aliezaliwa nje ya ndoa (isipokuwa ikiwa maiti akiacha wasia).
Chanzo:UADILIFU WA MIRATHI NDANI YA UISLAMU
Manswab Mahsen Abdul RahmaAl-Ridai Al- Jufry Uk 4