MAKATAZO KATIKA KUTAWADHA
1. Kuleta nia kwa sauti wakati wa kutawadha.
2. Kutumia maji kwa kupita kiasi.
3. Kuzidisha maosho matatu katika kutawadha, kwa riwaya iliyopokewa kuwa mbedui alikuja kwa Mtume ﷺ kumuuliza juu ya kutawadha, akamuonesha udhu mara tatutatu kisha akasema:
هَكَذَا الْوُضُوءُ، فَمَنْ زَادَ عَلَى هَذَا فَقَدْ أَسَاءَ وَتَعَدَّى وَظَلَمَ] رواه أبوداود والنسائي وأحمد]
[Kutawadha ni namna hii. Na mwenye kuzidisha hapo amekosea, amepita mpaka na amedhulumu] [Imepokewa na Abu Daud na Annasai na Ahmad.]
Lakini inafaa kuongeza zaidi ya maosho matatu iwapo atakuwa hakukisafisha kiungo kwa maosho matatu, kama mtu aliyeingiwa na mafuta au kitu kingine mkononi.
4. Kutoeneza maji katika kutawadha, kwa riwaya iliyopokewa kuwa mtu alitawadha, akaacha paku kadiri ya ukucha kwenye nyayo, Mtume ﷺ akaliona na aksema: [Rudi utawadhe kwa uzuri] [ Imepokewa na Muslim.] akarudi kisha akaswali.
Na inaingia kwenye kukosa kueneza maji ya udhu:
a- kutoosha vifundo viwili vya miguu
b- kutoosha visukusuku kwa sababu ya wembamba wa mikono ya kanzu.
c- kutoosha weupe ulioko baina ya masikio na ndevu.
d- Kutoosha kitanga cha mkono wa kushoto pamoja na mkono wa kushoto.
e- mwenye kutawadha naye una mapaku ya mafuta.
f- kutawadha kwa mwanamke na juu ya vidole vyake pana pambo lenye kuzuia maji kufika kwenye ngozi.
g- kutofikisha maji kwenye vidole vya miguu iwapo maji hayapiti baina ya vdole.
5. Kupangusa shingo:
Si miongoni mwa matendo ya kutawadha,
6. kuleta dhikiri ambazo hazikuja katika Sheria, mfano:
a- kuomba dua maalumu katika kuosha kila kiungo.
b- kumwambia “zamzam” mwenye kutawadha.