0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAANA YA KUOGA JANABA NA DALILI YAKE

MAANA YA KUOGA JANABA NA DALILI YAKE

MAANA YA KUOGA

Neno Kuoga au Josho ni matokeo ya tafsiri ya neno la kiarabu GHUSLU.

Neno hili lina maana mbili; ya kilugha na kisheria.

Kwa mtazamo wa kilughakukoga  ni kuyatiririsha maji kwenye kitu chochote kile kiwacho. Na Maana ya kisheria ni kitendo cha kuyapitisha maji mwili mzima kwa nia maalum kwa kusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu 

HUKUMU NA DALILI YA KUOGA JANABA:

Kuoga janaba kisheria ni Wajibu kwa kila Muislamu akipatwa na mojawapo wa mambo yatakayomlazimisha kukoga kama vile janaba kwa jimai au kukoga, hedhi, nifasi, uzazi na mengineyo kama tutakvyoeleza huko mbele.

Ulazima huu akipatwa na mambo haya ni juu ya kila Muislamu, mwenye akili timamu na mwenye uwezo wa kulitekeleza josho hilo.

Dalili na ushahidi wa Kuoga ni neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُواْ}       المائدة:5}

[Na mkiwa na janaba basi ogeni.]    [Al Maaida:6]

Na amesema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu:

وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ}     البقرة:222}

[Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu. Basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi. Wala msiwaingilie mpaka wat’ahirike.]     [Al Baqara:222]

Na dalili za usheria wa Kuoga zinapatikana ndani ya Qur’ani Tukufu, Sunna ya Mtume (Hadithi) na Ijmaai.

Miongoni mwa dalili za josho katika Qur’ani Tukufu :

{إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ التَّوَّابِينَ وَيُحِبُّ الْمُتَطَهِّرِينَ}    البقرة:222

[Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanao tubu na huwapenda wanao jisafisha ]    [Al Baqara:222].

Na Katika jumla ya dalili za Kuoga katika sunna ni ile hadithi iliyopopkelewa na Abu Hurayrah radhi za Allah ziwe juu yake amesema, amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:

[حق على كل مسلم أن يغتسل في كل سبعة أيام يومًا يغسل فيه رأسه وجسده]     متفق عليه

[Ni haki ya kila Muislamu kukoga siku moja katika juma, akaosha kichwa na mwili wake]

[Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Mapendeleo na muradi wa neno haki ni kwamba haifai kwa muislamu kuacha, na wanazuoni wameichukulia siku hiyo kuwa ni siku ya ijumaa.

Ijmaa ya wanazuoni mujitahidi imekongomana na kukubaliana kwamba kukoga kwa ajili ya nadhafa ni jambo lililosuniwa na kukoga kwa ajili ya kusihi ibada ni wajibu na hakuna hata mwanachuoni mmoja aliyelipinga kongamano hili.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.