0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAISHA YA ‘UMAR (Radhi za Allah ziwe juu yake) KATIKA ZAMA ZA UTUME

MAISHA YA ‘UMAR (R.A.) KATIKA ZAMA ZA UTUME

Alikuwa ‘Umar (r.a.) ni mshauri wa Mtume ﷺ kama alivyokuwa Abu Bakar (r.a.). Na alikuwa akiwa na Mtume ﷺ mda wote. Na alishuhudia vita vyote vya jihadi wakati wa Mtume ﷺ. Naye ana makubwa aliyoyafanya katika vita vya Badri na Uhud kisha vita vya Muraysi’.

Na pia yeye aliongoza kikosi kilichotumwa huko Turbah Kusini Mashariki mwa Makkah; na katika Sulhul-Hudaibiyah aliweka kumbu kumbu alipomwambia Abu Jandal bin Suhail bin ‘Amru akimnasihi: “Subiri ewe Abu Jandal, hakika hao ni washirikina.” Na ‘Umar (r.a.) alikuwa ni mmoja wa walioshuhudia mkataba wa suluhu ya Hudaibiyah .

Na katika vita vya kufutahi Makkah baada ya wanaume kumbayi’ Mtume ﷺ, walikusanyika wanawake wa Kiquraish wakiongozwa na Hind mke wa Abu Sufyan, ‘Umar (r.a.) alihudhuria mkutano huo, akacheka wakati Hind akijadiliana Mtume ﷺ. Akasema Mtume (s.a.w.) kumwambia ‘Umar: “Wabayi’ ewe ‘Umar (r.a.),” na ‘Umar (r.a.) akawabayi’ kuwa wao hawatomshirikisha Allah na kitu chochote wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawauwa watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaouzusha tu wenyewe baina ya mikono na miguu yao, wala hawatoasi katika mambo mema. [At- Terikhul-Islemv 3/137].

‘Umar (r.a.), binti yake Hafsah alipofiwa na mumewe, Khunais ibn Hudhafah As-Sahmy alimuoza Mtume (s.a.w.) katika mwaka wa Tatu wa Hijrah. Na aliposikia ‘Umar (r.a.) kuwa binti yake anamjadili Mtume ﷺ alimnasihi na kumtahadharisha na adhabu ya Allah pamoja na hasira za Mtume ﷺ, akatulia.

Na amepokea Ibn Majah kwa sanadi sahihi kutoka kwa Ibn Abbas (r.a.) kuwa amesema: “Amenihadithia ‘Umar (r.a.) kuwa amesema:” “Niliingia kwa Mtume (s.a.w.) nikampata amelala juu ya mkeka”. Akasema ‘Umar (r.a.): “Nikakaa chini, kwa ghafla nikamuona Mtume ﷺ amevaa kashida yake na wala hakuvaa kitu chengine, nikaona alama ya mkeka katika ngozi yake, na pia nikaona kiasi cha pishi moja ya sha’iir (ngano) katika pembeni mwa chumba na pia nikaona ngozi ya zamani imetungikwa katika nyumba ya Mtume ﷺ. Yakaanza macho yangu kutoa machozi.” Kisha Mtume (s.a.w.) akamuuliza: “Ni kipi kinachokuliza, ewe Ibn Al-Khattab?” Nikasema: “Ewe Mtume wa Allah, kwa nini nisilie na mkeka umekuweka athari mbavuni mwako, na pia katika khazina yako sioni ila hivi nivionavyo; na ilihali Kisra (mfalme wa Fursi) na (Qaysar mfalme wa Rumi) wako katika starehe ya matunda na mito, na wewe ni Mtume wa Allah Kipenzi chake akiba yako ni kama hii?” Akasema Mtume ﷺ:

[أَوَمَا تَرْضَى يَا عُمَرُ أَنْ تَكُونَ لَهُمُ الدُّنْيَا وَلَنَا الآخِرَةُ ؟]

[Ewe Ibn AI-Khattab huridhiki iwe Akhera ni yetu sisi, na dunia ni yao?]     [Hayatus- Sahabah 2/272 . ]

Na alikuwa ‘Umar (r.a.) mara nyengine akitoa rai mbele ya Mtume ﷺ, baadaye huteremka Wahyi kuwafikia rai yake. Miongoni  mwa rai zake alizozitoa kisha ukashuka Wahyi, ni kuhusu pombe na kubisha hodi. Basi si ajabu yeye kusifiwa na Mtume ﷺ kwa kusema:

[إن الله جعل الحق على لسان عمر وقلبه]

[Hakika Allah amejaalia haki katika ulimi wa ‘Umar na moyo wake]

na yeye ni Faruoq, ambaye kumpitia yeye Allah ﷻ amepambanua baina ya haki na batili.” [Khulafaur-Rashidun uk. 39]

Kwa Kifupi ‘Umar (r.a.) alikuwa ni mtu wa pili kwa ubora baada ya Abu Bakar (r.a.) kwa Mtume ﷺ na Masahaba (r.a.).

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.