SOMO LA FIQHI
Suala: Ni Maana ya nguzo.?
Jawabu: Nguzo ya kitu ni ile sehemu ya msingi ya kitu hicho kama vile kuta, na msingi katika nyumba.
Kwa hivyo nguzo za Swala ni zile ambazo Swala haikamiliki wala haisihi ila kwa kupatikana nguzo hizo.
Na Mtu akiacha nguzo moja ya swala kwa kukusudia basi Swala yake itabatika haitasihi,na ikiwa ameacha kwa kusahau basi itamlazimu ailete ile Nguzo kisha alete Sijdatu Sahwu.
Na ikiwa mtu amesahu kuleta Takbri ya kuhirimia Swala katikati ya swala itambidi aileta takbri ya Ihramu,na asihisabu ile rakaa aliyoiswali, kwa sababu Swala yake haikufungika,na ikiwa atakumbuka baada ya Swala itambidi aswali tena kwa sababu Swala yake ni batil,Haikufungika.
TAFAUTI KATI YA NGUZO NA MASHRTI
Sharti ni ile ambao yatakikana ipatikane kabla hujaingia katika kitendo cha Ibaada, mfano wa swala katika miongoni mwa sharti zake ni kuingia wakati wa Swala, kwa hivyo huwezi kuswali kwanza ni lazima uingie wakati wa Swala kisha ndio uswali.
Ama Nguzo ni ile ambao imefungamana na kitendo cha Ibaada mfano wa Rukuu na Sijda katika Swala na mfano wa hayo.