June 22, 2021
0 Comments
MAANA YA IHARAM
Suala: Ni nini Maana ya ihram (Kuhirimia)
Jawabu: Maana ya Ihram kilugha: Ni kuzuia
Ama maana ya Kuhirimia kisheria:
“Ni nia ya kuingia kwenye ibada ikifungamana na mojawapo ya matendo ya Hijja”
Na haifungamani Iharamu ila kwa nia, Mtu hahisabiwi kuwa amehirimia kwa kule kuazimia kwenda hijja au Umra kwa sababu toka aliposafiri mji wake huwa ameazimia kuhiji au kufanya umra, na wala hawi ni mwenye kuhirimia kwa kuvaa ihram au kuleta talbiya bila kutia nia ya ibada ya hijja kwa neno lake Mtume ﷺ :
[إنما الأعمال بالنيات وإنما لكل امرئ ما نوى] متفق عليه
[Hakika amali zote ni kwa nia na kila mtu hulipwa kama alivyo nuiya] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].