NI KWANINI UKAITWA USIKU WA CHEO (usiku waheshima)??
Kwanini ukaitwa usiku wa cheo (usiku waheshima)?
Wanachuoni wameeleze sababu ya kuitwa usiku huu wa Laylayul na miongoni mwa sababu walizozitaja ni haya yafuatayo
1. Kumesemwa: Ni kwasababu ya kuutukuza, kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ} {الأنعام:91}
[Na (Mayahudi ) hawakumhishimu Mwenyezi Mungu kama inavyotakiwa kumhishimu] [Al-An-a’m – Aya 91].
Na maana yake: Ni kwamba huu usiku ni wenye hishima; kwa kuteremshwa Qur’ani ndani yake na kupatika na kushuka malaika, na ni usiku wa baraka na rehema na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
2. Inasemekana: Al-qadr kwa maana ya kubanika kwa kuwa ndogo sana, kama kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{وَمَن قُدِرَ عَلَيْهِ رِزْقُهُ فَلْيُنفِقْ مِمَّا آتَاهُ اللَّهُ} {الطلاق:7}
[Na yule ambaye amepungukiwa riziki yake (riziki yake imebanika kwa kuwa ndogo sana), atoe katika kile alichopewa na Mwenyezi Mungu] [At-twalaq – Aya 7].
Na maana ya kubanika kwa kuwa ndogo sana: Ni kule kufichika katika elimu za watu kutambua hasa usiku huo ni usiku wa tarehe ngapi.
3. Na inasemekana: Al-qadr kumaanisha makadirio, kwa maana: katika usiku huu ndiyo kunakadiriwa hukumu za mwaka ulioko; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُّبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ} {الدخان 3-4}
[Hakika tumekiteremsha katika usiku ulio barikiwa. Hakika Sisi ni Waonyaji.Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima,] [Ad-Dukhan – Aya 3-4].