0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUSILIMU KWA ‘UMAR IBN AL KHATTWAB (R.A.)

KUSILIMU KWA ‘UMAR IBN AL KHATTWAB (R.A.)

Alipotumilizwa Mtume ﷺ na kutangaza Uislamu kwa watu, basi waliingia wenye kuingia katika Uislamu. Na miongoni mwao katika jamii yake ni dada yake ‘Umar (r.a.) ambaye ni Fatimah na mtoto wa Ammi yake ambaye ni shemeji yake Sa’id ibn Zaid, na Nu’aym ibn Abdullah; na wengine kutoka katika Bani Adiy. Ama ‘Umar (r.a.) wakati huo alikuwa hajasilimu, na alikuwa mwenye kushikamana na itikadi yake ya kijahilia, akifanya uadui wa kuupinga Uislamu jambo ambalo alilolitoa kutoka kwa mjomba wake Abu Jahl. Na alikuwa katika watu ambao wanapinga kuendelea kwa Uislamu, na akiwaudhi ambao wameingia katika Uislamu na kuwapiga watumwa na madhaifu kati yao.

Na Mtume ﷺ alikuwa amemuomba Mwenyezi Mungu amuongoze ‘Umar katika Uislamu. Amepokea Tirmidhi kutoka kwa ibn ‘Umar (r.a.) kwamba Mtume ﷺ amesema:

[اللهم أعز الإسلام بأحب هذين الرجلين إليك]

[Ewe Mola upe nguvu Uislamu kupitia kwa mmoja unayempenda zaidi katika watu wawili hawa] ‘Umar ibn AI-Khattab au Abu Jahl ibn Hisham. Ikawa apendwaye zaidi na Mwenyezi Mungu ni ‘Umar. [At- Tirmidhi Juz.2/209]

Alitoka ‘Umar (r.a.) siku moja huku akishika upanga wake, akikusudia kwenda kumuuwa Mtume ﷺ. Akakutana njiani na Nu’aym ibn ‘Abdullah (r.a.), wakajadiliana, akageuza safari yake akaelekea hadi nyumbani kwa shemeji yake Sa’id ibn Zaid akiwa pamoja na mkewe Fatimah (r.a.), ambaye ni dada yake ‘Umar (r.a.). Akawapata wanasoma ukurasa ambao ndani yake kuna Surat Twahaa.

Akawapiga na kuwajeruhi mpaka wakasema: “Ndio tumesilimu na tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, fanya utakalo.” Baada ya kusikia maneno hayo ‘Umar akaathirika, akautaka ule ukurasa ambao walikuwa wakiusoma, dada yake akakataa kumpa akamwambia: “Sisi tunachelea kukupa huo ukurasa.” Akajibu ‘Umar kumwambia dada yake: “Usiogope” na akaapa kuwa hatafanya ubaya. Akatumai dada yake kuwa huenda akasilimu akamwambia: “Ewe kaka yangu hakika wewe ni najisi kwa ajili ya shirki yako, na huu ukurasa hauguswi ila na aliyetahirika.” Akaenda ‘Umar kuoga kisha dada yake akampa ule ukurasa, akausoma. Kisha akasema: “Ni uzuri ulioje wa maneno haya!” Kisha akaenda mpaka kwenye nyumba ya Al-Arqam ibn Al-Arqam, huko Safaa ambako ni makao ya Mtume ﷺ na Masahaba wake. Alipowasili ‘Umar (r.a.) akasema kumwambia Mtume ﷺ “Ewe Mtume wa Allah nimekujia nipate kumwamini Allah na Mtume Wake pamoja na yale yaliokuja kutoka kwa Allah.”

Mtume ﷺ akapiga Takbir ambayo iliwajulisha watu wa nyumba ile kuwa ‘Umar amesilimu. Alisilimu ‘Umar baada ya Hamzah kwa siku tatu, mwishoni mwa Mwezi wa Mfungo Tatu mwaka wa sita kutoka kutumilizwa Mtume ﷺ  Na ‘Abdullah Ibn Mas’ud alikuwa akisema: “Hatukuwa tukiweza kusali Al-Ka’ba mpaka aliposilimu ‘Umar ibn AI-Khattab, aliposilimu aliwapiga vita Maquraish mpaka akaweza kusali kwenye Al-Ka’ba na tukasali pamoja naye.”

Na imepokewa kuwa Mtume ﷺ alitoka siku moja na Masahaba zake katika safu mbili, Umar (r.a.) akiwa mbele ya safu moja na Hamzah (r.a.) akiwa mbeie ya safu hiyo nyingine mpaka wakaingia msikitini, ‘Umar na Hamzah wakafika kwa Maquraish. Maquraish wakawaangalia na kupatwa na huzuni ambayo haijawahi kuwapata. Mtume ﷺ akamwita ‘Umar kuanzia siku hiyo Al-Faruq.

Pamoja na kuwa ‘Umar (r.a.) alikuwa ni mtu mwenye utisho na ni mwamba, pia hakuwa mwenye kunusurika na mateso ya Ma’quraish mpaka wakaweza kumshambulia wakawa wanampiga nave akiwapiga, mpaka ‘Umar (r.a.) akachoka kupigana nao na akakaa chini, wakamsimamia Maquraish na kumpiga kichwani na huku

akiwaambia: “Fanyeni mtakacho, naapa kwaMwenyezi Mungu, lau si si walstamu tungekuwa idadi yetu mia tatu, hakika si si tungewaachia nyinyi huu mji au nyinyi mungetuachia sisi .” [Sirat Ibn Hisham 1/474]

*Al Khulafaau Arrashidun 59-61

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.