June 17, 2021
0 Comments
KUSILIMU KWA ABU BAKAR RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE
Wameafikiana wanazuoni wa tarekhe kuwa Abu Bakr (r.a.) ni wa kwanza kusilimu katika wanaume, kwa vile alikuwa akijua mwenendo wa Mtume ﷺ na tabia zake njema, kama vile ukweli, uamtnifu na Uchaji Mungu, na ni wa kufaa kubeba ujumbe utokao mbinguni, (Uislamu), basi alipolinganiwa na Mtume ﷺ aingie katika Uislamu, Abu Bakr (r.a.) hakutia shaka juu ya jambo hilo, bali alipiga shahada kwa kusema:
[ أشهد أن لا إله إلا الله وأشهد أنك رسول الله]
[Hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.]