SOMO LA FIQHI
MAANA YA KHOFU
Khofu ni neno la Kiarabu ambalo hutumika kwa maana ya aina maalumu ya kiatu chenye umbo la soksi.Viatu hivi vinaweza kuwa ni vya ngozi au malighafi nyingine ifananayo na ngozi kama vile kitambaa kigumu.
Mojawapo ya misingi iliyojengewa sheria ya Kiislamu ni Wepesi.Siku zote uislamu huwatakia wepesi na urahisi wafuasi wake katika utendaji na utekelezaji wao wa ibada na matendo yao ya maisha ya kila siku.Ni kwa kuuzingatia msingi huu ndipo hutaweza kukuta hata mara moja uislamu umeweka sheria isiyotelelezeka.
Mwenyzi Mungu Mtukufu anasema:
{وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ} الحج:78
[Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini] [Suratul Hajj:78]
Kwa sababu huu Uislamu umemjuzishia na kumruhusu muislamu kupakaza maji juu ya khofu badala ya kuosha miguu wakati wa kutawadha kwa masharti makhususi tutakayoyaona hapo baadae.
Na Ruhusa hii ni kwa wanamume na wanawake pamoja na itatumika mtu awapo safarini au mjini.
Kupakaza maji juu ya khofu kumethibiti katika suna tukufu ya Bwana Mtume ﷺ.
Miongoni mwa hadithi zilizothibiti katika mas’ala haya ni Hadithi hizi zifuatazo:
1. Imepokelewa na Al Mughyrah Ibn Shu’ubah Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ Amesema:
كُنْتُ مَع النّبيِّ – صلى الله عليه وسلم ، فَتَوَضَّأَ، فَأَهْوَيْتُ لأنْزِعَ خُفّيْهِ، فَقَالَ: دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ، فمَسَحَ عَلَيْهِمَا] متفق عليه]
Nilikuwa pamoja na Mtume ﷺ Akatwadha nikaporomoka (nikainama) ili nimvue khofu zake, mtume akasema: [Ziache, kwani mimi nimezivaa il hali (miguu) ikiwa twahara, Akapakusa juu yake] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
2. Hadithi iliopokelewa na Anas Rahi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:
[إذا توضأ أحدكم ولبس خفيه فليصل فيهما وليمسح عليهما ،ثم لا يخلعهما إن شاء إلا من جنابة] رواه الدارقطني
[Atakapotawadha mmoja wenu , kisha akavaa khofu. (Atakapotawadha tena) basi na apakaze maji juu yake (hizo khofu) na wala asizivue akitaka (kufanya hivyo) ila akipatwa na janaba.] [Imepokea na Al Daaruqutwiy]