0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUOGOPA NA KUTARAJI

KUOGOPA NA KUTARAJI

Nini kuogopa? Na nini kutaraji ?
Kuogopa ni tafsiri ya kuumwa moyo na kuchomeka kwa sababu ya kuingia katika jambo la karaha, la kuchukiza. Mfano; mtu akafanya kosa mbele ya mfalme kisha likamchukia moyoni kwake kwa kuogopa kufa na ikawa anajua kuwa inafaa kusamehewa na muogopaji zaidi ni yule anayeiogopa nafsi yake. Mtume ﷺ Amesema:

[إِنَّ أَتْقَاكُمْ وَأَعْلَمَكُمْ بِاللَّهِ أَنَا]    رواه البخاري

[Hakika mcha mungu zaidi na anae mjua zaidi Mwenyezi Mungu ni mimi]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim].

Kuogopa na kutaraji ni mbawa mbili wanarukia wenye kujikuribisha na kila jambo nzuri na ni kipando wanakaa kwa hizo njia mbili.

hakika vitendo vya moyo ni katika jambo kubwa na katika matukufu. Thawabu zake ni tukufu na ni kubwa na adhabu yake ni kubwa na vitendo vya viungo vinafuata vitendo vya moyo na vinajengwa juu yake. Kwa hivyo, ndiyo kukasemwa: Moyo ni mfalme wa viungo na baki ya viungo ni vijakazi wake.
Imepokewa na Anas radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie, akipokea kutoka kwa Mtume ﷺ Amesema:

[لا يستقيم إيمان عبد حتى يستقيم قلبه]    رواه أحمد

[Mja hatakuwa na msimamo wa Imani mpaka awe na msimamo na moyo wake]    [Imepokewa na Ahmad].
Maana ya msimamo wa moyo ni kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kumtukuza, kumpenda, kumuogopa, kumtaraji, kupenda twaa yake na kuchukia maasi yake.
Amepokea Muslim kutoka kwa Abu Hurayra Amesema; Amesema Mtume ﷺ:

[إِنَّ الله لا يَنْظُرُ إِلى أَجْسامِكْم، وَلا إِلى صُوَرِكُمْ، وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ]    رواه مسلم

[Hakika Mwenyezi Mungu haangalii miili yenu wala sura. Lakini ataangalia nyoyo zenu].   [Imepokewa na Muslim]

Amesema Al-Hassan kumuambia mtu: ‘Ufanyie dawa moyo wako, hakika haja ya Mwenyezi Mungu kwa waja ni kutengea nyoyo zao. Na hakika vitendo vya nyoyo ambazo zinapelekea vitendo vizuri na huvutia nyumba ya akhera, na hukemea vitendo vibaya na hupa mgongo ulimwengu na huchukia nafsi mbaya illiyoaswi ni kuogopa na kutaraji.
Na makusudio ya kuogopa ni kupiga moyo na kubabaika na kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwa kutofanya mambo ya haramu au kuacha jambo la wajibu au kuwa na kasoro katika mambo mazuri. Vilevile, ni katika kuogopa kuwa na hamu ya kutokubali Mwenyezi Mungu vitendo vyako, ikatetemeka nafsi na mambo ya haramu na kukimbilia mambo ya kheri. Amesema Ibnul-Qayyim Mwenyezi Mungu amrehemu : ‘Kuogopa ni kwa Waislamu wote na kicho ni kwa wanavyuoni wanaojua ‘.
hakika Mwenyezi Mungu Amemuahidi mwenye kumuogopa yeye, kumzuia yeye na matamanio na kumsaidia katika Twaa na kumlipa malipo bora. Amesema Allah (Subhaanahu wa Taala):

{وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ جَنَّتَانِ فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ ذَوَاتَا أَفْنَانٍ}    الرحمن:46-48

[Yule anaemuogopa mola wake atapata mabustani mawili. Ni yapi katika neema za Mwenyezi Mungu munakanusha? mabustani yenye miti yenye matawi mengi]    [Arahmaan : 46 – 48].

Tuangalie watu wema namna walivyokua wakimuogopa Mwenyezi Mungu na kumtarajia. Ilikua kuogopa kwao ni hali ya juu wakifanya vitendo vizuri na kutaraji rehma ya Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, kuogopa iliwatengeneza na wakasafisha vitendo vyao na yakawa mazuri maregeo yao. Amesema Abu Hafsi: ‘Kuogopa ni kibati cha Mwenyezi Mungu huwanyosha waliokimbia mlango wake’. Na akasema : ‘kuogopa ni taa katika moyo’.
Nakumuogopa Mwenyezi Mungu inapelekea kufanya mambo ya akhera na ni ngome ya kila jambo. Inamsukuma mja kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na malipo yake. Inapelekea kuwa na hima ya juu kufanya vitendo vizuri.
Kumuogopa Mwenyezi Mungu huzuia nafsi na shahwa zake na huikemea na upotevu na inamuhami kumpelekea kwa kila jambo zuri na kufaulu. Na kumuogopa Mwenyezi Mungu ni sehemu katika sehemu za kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, inafaa iwe kuogopa kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu ni sehemu katika sehemu ya shirki kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Na ameamrisha Mwenyezi Mungu kumuogopa yeye katika Aya nyingi na akakataza kumuogopa asiyekuwa yeye. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

{إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ} آل عمران:175

[Hakika huyo ni Shet’ani anawatia khofu marafiki zake, basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.]    [Al-Imran : 175].
Na katika Hadithi za Mtume ﷺ. Imepokewa na Anas radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie Amesema: Alikuja Mtume ﷺ Akasema:

[لَوْ تَعْلَمُونَ مَا أَعْلَمُ لَضَحِكْتُمْ قَلِيلًا وَلَبَكَيْتُمْ كَثِيرًا]    رواه البخاري ومسلم

[Lau mgejua ninayo yajua mgalicheka kidogo na mkalia kwa wingi]. Masahaba wakajifunika nyuso zao wakatoa koromo za kilio.   [imepokewa na Bukhari na Muslim].

Kwa hivyo muislamu ni lazima awe nimwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu (Subhanahu wata’ala) wala asiwe ni mtu asie jaili kufanya analo taka kisha akawa na matarajio mazuri,na vile vile asiwe ni mwenye Kutegemea matendo yake peke yake kuwa ndio yatakao muingiza peponi bali nilazima awe na khofu na kuwa huenda matendo yake haya kukubaliwa,na kadhalika asiwe ni mwenye kukata tamaa na Rehema za Mwenyezi Mungu hata akawa ni mwenye Madhambi mengi,ni awe na matarajio mema na atende yalio Mazuri hii ndio mtu kuwa na khofu na raja ya Mwenyezi Mungu (Subhanahu wata’ala).

Amesema Ibnu Rajab Mwenyezi Mungu Amrahau : ‘Kiasi kinacho faa kutokana na kuogopa ni iliyo msaidia mtu kutekeleza jambo la lazima na kujiepusha na mambo ya haramu. na ikiwa juu hapo; nao ni kupelekea nafsi kufanya bidii kufanya Twaa ya ziada na kujizuia na yenye kuchukiza na kukunjua itakuwa ni yenye kupendeza. Na ikizidi juu ya hapo linarithisha magonjwa au kufa kwa moyo. Na kusababisha nafsi kukataa kukimbilia vitendo vizuri na hili si jambo lakupendeza.
Baada ya hapo tuangalie kutaraji nayo ni kuwa na tama kwa malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu juu ya kufanya vitendo vyema. Na sharti ya kutaraji ni kutanguliza vitendo vizuri na kujizuia na mambo ya haramu. Ama kuacha ya wajibu na kufuata matamanio na kutamani malipo kwa Mwenyezi Mungu na kumtarajia yeye, hapo itakua ni kutaka amani na adhabu ya Mwenyezi Mungu na wala si kutaraji. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى: {أفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّهِ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ}     الأعراف: 99

[Hawaaminishi adhabu ya Mwenyezi Mungu ila watu waliopata hasara]     [Al-Araaf:99].

Ndugu Muislamu: Jua ya kwamba kutaraji bila vitendo ni kujidanganya.

Na Mwenyezi Mungu amekataza Hilo. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala):

قال تعالى : {يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُمْ بِاللَّهِ الْغَرُورُ}    فاطر: 5

[Enyi watu hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, basi yasiwadanganye maisha ya kilimwengu wala Yule mdanganyaji mkubwa (Iblis) na sikudanganyeni juu ya Mwenyezi Mungu] [Fatir: 5].

Mwisho

Ndugu Muislamu tumuogope Mwenyezi Mungu na tutarajie kheri kutoka kwake. Natuogope adhabu yake ili tupate malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu malipo ya akhera na dunia. Mwenyezi Mungu atujalie ni wenye kumuogopa yeye na kumtarajia yeye, na atupe kheri ya dunia na akhera atujalie ni katika wenye kusikia mema na kuyafuata, na mabaya tuyaepuke.

 SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH ALI BAHERO 

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.