0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUMTAKASIA MWENYEZI MUNGU IBAADA

KUMTAKASIA MWENYEZI MUNGU IBAADA

Nini Ikhlasi? Ikhlasi ina maana nyingi; Kuna wanao sema: Ikhlasi ni kuwa sawa ndani ya mwanaadamu na nje yake. Wengine wasema: Ikhlasi n ikufanya vitendo bila yakujionesha. Na mtu yoyote anayefanya vitendo vyoyote bila ya kujitakasa, vitendo vyake havikubaliwi. Kwasababu Ikhlasi ni nguzo muhimu ya kukubaliwa vitendo, Na kwa sababu ya Ikhlas huzidishiwa daraja mtu.

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) hakubali vitendo ila viwe ni vyema vimefanywa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Mwenye kufanya vitendo na akamshirikisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) kwa kumkusudia mtu mwengine asiyekuwa Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), Mwenyezi Mungu Mtukufu hakubali amali yake, hata amali hiyo iwe nyingi kiasi gani. Dalili katika hayo ni maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu Aliposema:

{إِنَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ فَاعْبُدِ اللَّهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ}     الزمر:2

[Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa Haki. Basi muabudu Mwenyezi Mungu ukimsafia Dini Yeye tu].    [Az-zumar 2].

Enyi Waislamu jueni ya kuwa vitendo vyote lazima viwe na (Ikhlas) kujitakasa. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukuf:

{قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۚ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ}    الأعراف:29

[Sema: Mola Mlezi wangu ameamrisha uadilifu, na mumuelekeze nyuso zenu kila mnapo sujudu, na muombeni Yeye kwa kumsafia Dini. Kama alivyo kuumbeni mwanzo ndivyo mtavyo rudi]   [A- Araf : 29].
Amesema tena Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ} البينة:5

[Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini, wawe waongofu, na washike Sala, na watoe Zaka. Na hiyo ndiyo Dini madhubuti.]   [.Bayyina: 5].
Sifa na vitendo vyote vilivyo mbali na ikhlasi havikubaliwi na Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala). Ewe mja wa Mwenyezi Mungu ni kukusudia vitendo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu peke yake wala usimshirikishe na chochote ndio utapata malipo kutoka kwa Allah.
Zingatia Ewe Muislamu ni vipi Qur’an ina muombea mwenye kuisoma, pamoja na kuwa Qura’n ni maombezi siku ya kiyama lakini hapa haikumuombea kwa sababu ya kukosa ikhlas. Ni hivyo hivyo mali hayamuombei mwenye mali kwa kufanyia watu wema kuunga kizazi kwa sababu ya kukosa ikhlas. Na vile vile aliyepigana vita lakini kupigana kwake hakukumsaidia Allah. Kwa sababu alikuwa mbali na ikhlas. Je mimi na wewe tuko wapi? Ole wetu tukihalifu ikhlas ambayo ni nguzo kubwa ya kukubaliwa vitendo.

MAMBO YANAYO HARIBU IKHLASI:

A) Kumshirikisha Mwenyezi Mungu sawa kwa shiriki ndogo au kubwa.
(1) Shirki kubwa : Ni kuthibitisha mshirika wa Mwenyezi Mungu kwa kukusudiwa mwingine. Na Shirki hii inamtoa mtu kwenye dini, na kwasababu ya shirki ataingia motoni na atabaki humo milele na shirki kubwa hubatilisha na kuharibu vitendo yote.
(2) Shirki ndogo: nayo ni kila neno au kitendo kilicho kusudiwa kuonyesha watu. Shirki hii haimtoi mtu katika dini kama kujionesha kutaka sifa.
Na hio ni mbaya kwa muumin, kwasabau inakanusha ikhlas na inabatilisha vitendo ambavyo vimepatikana kwa kujionesha sio kwa ajli ya Allah. Imepokewa na Mahmuod Ibnu Labidi ya kwamba Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) Amesema:

إِنَّ أَخْوَفَ مَا أَخَافُ عَلَيْكُمْ الشِّرْكُ الْأَصْغَرُ] قَالُوا وَمَا الشِّرْكُ الْأَصْغَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ قَالَ:[الرِّيَاءُ يَقُولُ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ لَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِذَا جُزِيَ النَّاسُ بِأَعْمَالِهِمْ اذْهَبُوا إِلَى الَّذِينَ كُنْتُمْ تُرَاءُونَ فِي الدُّنْيَا فَانْظُرُوا هَلْ تَجِدُونَ عِنْدَهُمْ جَزَاءً      رواه أحمد والطبراني

[Ni nalo waaogopea juu yenu ni shirki ndogo wakasema ni ipi shirki ndogo?. Akasema: ni Riya.

Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) atawaambia wao siku ya kiyama atakapo walipa watu kwa vitendo vyao: Nendeni kwa wale mliyo kuwa mkijionesha katika dunia muangalie mtapata malipo kwao]      [Imetolewa na Ahmad na Al Twabraaniy].

B) Kukusudia Dunia kupitia vitendo vya akhera. Nayo nikufanya baadhi ya vitendo vya akhera kwa ajili ya kupata starehe za ulimwengu. Mfano anae pigana kwa ajili ya kupata Ghanima mali ya makafiri, au kufundisha ilimu ya Dini kwa sababu ya kupata Shahada cheti au kupata kazi. Na hayo kuna hali mbili:
(1) Ikiwa kutaka ulimwengu kwa kitendo cha akhera ni chenye kukusudiwa kwa ajili ya ulimwengu, au kikawa ni sawa sawa na kusidio ya akhera. Kufanya hivyo, inapelekea kuharibu ikhlasi, bali inapelekea kupata dhambi, na kubatilisha vitendo vyote. Amepokea Ubayyah Ibnu Kaab akisema; Amesema Mtume ﷺ:

بَشِّرْ هَذِهِ الْأُمَّةَ بِالسَّنَاءِ وَالرِّفْعَةِ وَالدِّينِ وَالنَّصْرِ وَالتَّمْكِينِ فِي الْأَرْضِ ، فَمَنْ عَمِلَ مِنْهُمْ عَمَلَ الْآخِرَةِ لِلدُّنْيَا ، لَمْ يَكُنْ لَهُ فِي الْآخِرَةِ نَصِيبٌ]    رواه أحمد

[Wape bishara umma huu kwa utukfu na kunusurika kwa dini na kuamikinika katika Ardhi, Mwenye kufanya katika wao kitendo cha akhera kwa ajili ya ulimwengu, hatakuwa na  fungu siku ya akhera]   [Imepokewa na Ahmad]

Ewe Mwenyezi Mungu takasa vitendo vyetu na shirki, na utujaalie kuwa na ikhlasi katika Matendo yetu ya dhahiri na yasiri.

MATUNDA YA IKHLASI

Kumtakasia Mwenyezi Mungu Ibaada kuna faida nyingi sana miongoni mwa faida ya Ikhlasi ni haya yanayofuata:
1) Ni kuthibitisha tawhidi na Akida ya Muislamu, pamoja na kusalimika na unafiki.
2) Kuingia Peponi na kuepukana na moto. Na Muisilamu anapo ingia motoni ni kuwa hakuwa na Ikhlasi katika Matendo yake.
3) Kukubaliwa vitendo na kuongezewa malipo.
4) Kusamehewa madhambi
5) Kuonja utamu wa ibada na daraja zake.
6) Kufaulu kupata uombezi wa Mtume ﷺ siku ya akhera.
7) Kupata amani kwa ukamilifu, na uongofu duniani na ahkera
8) Kuhifadhiwa na fitna na vitimbi vya shetani.
9) Kumkomboa mja na ibada ya Shetani
10) Kufurahiwa na watu na kupendwa.
11) Kuepushwa moyo wake na uchafu wa kujiona kibri na hasadi.
12) Kupata nusra ya Mwenyezi Mungu.

Na alikuwa Mtume ﷺ Akijilinda kwa Mwenyezi Mungu kuingia katika shirki kwa sababu ya kukosa ikhlasi.
Anasema Mtume ﷺ: [Shirki imefichika kama ubawa wa chungu mweusi nitakujulisha jambo ukilifanya itakuwa kando na wewe shirki ndogo na kubwa. Sema:

[اللهم إني أعوذ بك أن أشرك بك شيئاً وأنا أعلم، وأستغفرك من الذنب الذي لا أعلم]    أخرجه أحمد

Ewe Mwenyezi Mungu, hakika mimi najilinda kwako na kukushirikisha hali najuwa, naomba msamaha kwako kwa nisilo lijuwa].    [Imepokewa na Ahmad]

Ewe Mwenyezi Mungu turuzuku ikhlasi katika maneno na vitendo.

Mwisho
Ewe ndugu Muislamu hakuna katika sisi asiye taka kufaulu. Basi tunapo taka kufaulu tushikamane na ikhlasi, kwani ikhlasi ni katika nguzo za kukubaliwa vitendo vyetu. Kama ilivyopokewa kutoka kwa maneno ya wanavyuoni sharuti zakukubaliwa matendo ni mbili: (1) Ikhlasi (2) Kumfuata Mtume ﷺ.

Tunakuomba Mwenyezi Mungu uturuzuku ikhlasi na utuepushe na kujonyesha katika vitendo vyetu. Ewe Mwenyezi Mungu tuhifadhi na utulinde kutokushirikisha wewe na kitu chochote.

KWA FAIDA ZAIDI SIKILA MADA HII NA SHEIKH HAMMAD QASIMA

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.