0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KULALA MUZDALIFA

SOMO LA FIQHI

1. Haji atakapofika muzdalifa atanza na Swala ataswali Maghrib na Ishaa kwa kuzikusanya na kupunguza Swala ya isha, kabla kuteremsha mizigo na vitu vyake.

2. Nilazima kulala Muzdalifa usiku wake na ataswali Alfajiri mapema, na haifai kuondoka muzdalifa kabla ya Alfajiri ila kwa wenye udhuru, kama watu madhaifu katika wanawake, na watoto na kwa wale wanaofuatana nawao, ambao wanawatumikia wao yafaa kuodoka nawao mwisho wa usiku Mwezi unapo zama.

3. Anapo maliza kuswali Alfajiri inapendekezwa kwa mahujaji aende kwenye Mash’aril haram, na aeleke kibla na azidishe dhikri na Dua hali yakuwa ameinuwa mikono yake na ataendelea kufanya hivyo mpaka kupambazuke sana, na sehemu yoyote atakapo simama Muzdalifa yafaa, kwa neno lake Mtume ﷺ:

[وقفت هاهنا وجمع كلها موقف]   رواه مسلم

[Nimesimama hapa na jam’u yote ni mahali pakisimamo]   [Imepokewa na Muslim]

na makusuduio ya Jam’u ni Muzdalifa.

4. Anapoondoka haaji kutoka muzdalifa inapendekezwa aokote vijiwe saba pekeyake kwa ajili yakutupa kwenye jamaraat, ama masiku yalio baki ataokota vijiwe mina au sehemu yoyote atakapo okota yafaa

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.