0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

IDUL-ADH’HA

IDUL-ADH’HA

Idul Adhaha (Iddi ya kuchinja) ni mojawapo ya idd mbili katika Uislamu na inakuwa tarehe kumi Dhulhijaa baada ya kusimama Arafa sehemu ambayo wamesimama mahujaj katika kutekeleza Hijja, na kwisha Iddi hiyo tarehe 13 Dhulhija. Iddi hiyo ni kukumbuka kisa cha Nabii Ibrahim alipotaka kumchinja mwanawe Ismail kwa ajili hiyo wanasimama Waislamu kuchinja wanyama.

Hekima ya Swala ya Iddi

Imeshurutishwa swala ya Iddi ili kuzishukuru neema za Mwenyezi Mungu na kushibisha matamanio ya binadamu.

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ}   الروم:30

Bali walio dhulumu wamefuata mapendo ya nafsi zao pasina kujua. Basi nani atamwongoa ambaye Mwenyezi Mungu amemuacha apotee? Wala hao hawatakuwa na wa kuwanusuru.”     [Al-Rruum:30]

Iddi ni Mkusanyiko wa Mambo Manne:

  1. Kukusanyika kwa watu.
  2. Kukusanyika kwa sehemu.
  3. Kukusanyika kwa wakati.
  4. Kukusanyika kwa ibada maalum.

Amesema Mwenyezi Mungu  Subhaanahu wa Taala:

{وَلِكُلِّ أُمَّةٍ جَعَلْنَا مَنسَكًا لِّيَذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَىٰ مَا رَزَقَهُم مِّن بَهِيمَةِ الْأَنْعَامِ ۗ فَإِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ فَلَهُ أَسْلِمُوا ۗ وَبَشِّرِ الْمُخْبِتِينَ}     الحج:34

Na kila umma tumewafanyia mahala pa kuchinjia mihanga ya ibada ili walitaje jina la Mwenyezi Mungu juu ya vile walivyo ruzukiwa katika wanyama wa mifugo. Basi Mungu wenu ni Mungu Mmoja tuJisalimishieni kwake tu, na wabashirie wanyenyekevu.”     [Al-Hajj:34]

Imepokewa na Anas (R.A.) kwa Mtume  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  alipokwenda Madina aliwakuta watu wa Madina wana siku mbili wanacheza, Mtume (Swalla Llahu ‘alayhi wasallam) akawaambia [Mwenyezi Mungu amekubadilishieni siku mbili hizi kwa iddul Adha(kuchinja) na Iddul-fitr (baada ya Ramadhani]

Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{فَصَلِّ لِرَبِّكَ وَانْحَرْ}      {الكوثر:2

Basi sali na uchinje kwa ajili ya Mola wako Mlezi.”    [Al-Kawthar:2]

Hukumu ya Kuchinja katika Siku ya Iddi Pamoja na Sharti Zake na Namna ya Kuchinja.

Amesema Ibnu ‘Umar (R.A.) “Kuchinja ni sunnah”. Na Amesema Imam Sha’abi: Mungu Amrehemu “ Haruhusiwi mtu kuacha kuchinja isipokuwa kwa mwenye kuhiji na kusafiri”.

Na Imepokewa na Ibnu Majah kwa Mtume  Swalla Llahu ‘alayhi wasallam ameamrisha kugawanya nyama ya Udhiya mara tatu akisema kuleni, toeni sadaka na muhifadhi.

Kushurutishwa Kupiga Takbira pamoja na Hukumu Zake na Namna yake

Imepokewa na Ibnu Abbas amesema Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam  [hakuna siku kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, wala siku zinazopendekezwa kwake amali kama siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhulhija, zidisheni Tasbihi na Takbiri na Tahlil (Lailaha ila Allah).]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.