0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

FADHLA YA KUFUNGA SIKU YA ASHURA’A

FADHLA YA KUFUNGA SIKU YA ASHURA’A

Mwezi wa (muharram) ni katika miezi mitukufu na ndio mwezi wa kwanza katika kalenda ya kiuslamu na tarehe 10 ya mwezi huu (Ashuuraa) ni siku adhimu na ina historia kubwa kwani siku hii ndiyo siku ambayo ALLAH alimuokoa Nabii (Mus a.s) na wana waisraeli kutokana na mateso na vitimbi vya fir’aun.Siku hii Mtume  aliwakuta maqureish wakifunga zama za ujahiliyyah na mtume alifunga kama ilivyo kuja kwenye hadithi iliyokelewa na Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesem:

[كان يوم عاشوراء تصومه قريش في الجاهلية، وكان رسول اللَّه صلى الله عليه وسلم يصومه في الجاهلية]    رواه البخاري ومسلم

 

[Ilikuwa siku ya Ashuraa maqurish wakifunga zama za ujahilihiya na alikuwa Mtume rehma na amani zimfikiyeye alikuwa akifunga zama za Al-Jaahiliyah.]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na Mtume ﷺ alikuwa akiwahimiz awaislamu kuifunga siku hii ya ashura kabla ya kufaradhiwa mwezi wa Ramadhani.

وعن قيس بن سعد بن عبادة رضي اللَّه عنه قال: ” أمرنا النبي صلى الله عليه وسلم أن نصوم عاشوراء قبل أن ينزل رمضان، فلما نزل رمضان، لم يأمرنا ولم ينهنا، ونحن نفعله .  أخرجه النسائي في الكبرى وأحمد

Kutoka kwa Qays bin sa’d bin Ubaada radhi za Allah ziwe juu yake asema: [Alituamrisha Mtume tufunge Ashuraa kabla ya kufardhiwa ramadhani,ilipo faradhiwa Ramadhani hakutuamrisha wala hakutukataza,na sisi tulikuwa tukifunga.]      [Imepokewa na Al-Nnasaai na Ahmad]

Na Mtume alivyokwenda Madina aliwakuta mayahudi wanafunga siku hii alivyowauliza wakasema hii ndio siku ambayo ALLAH alimuokoa Nabii wetu Musa kutokana na fir’aun kwahivyo musa alifunga kwa kumshukuru ALLAH na sisi twafunga kwa kumshukuru ALLAH kumuokoa Nabii wetu na fir’aun.kama ilivyo pokelewa Kutoka kwa Ibnu Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake asema:

” قدم رسول اللَّه صلى الله عليه وسلم المدينة فرأى اليهود تصوم يوم عاشوراء، فقال: ما هذا؟ قالوا: هذا يوم صالح، نجّى اللَّه فيه موسى وبني إسرائيل من عدوهم، فصامه، فقال: أنا أحق بموسى منكم فصامه وأمر بصيامه.      رواه البخاري ومسلم

Mtume  ﷺ alipokwenda Madina aliwaona Mayahudi wakifunga siku ya Ashura’a akauliza ni saumu gani hii ? wakasema: Hii ni siku bora Mwenyezi Mungu alimuokowa nabii Musa na wana Waisrail kutokana na adui yao,(Musa) akafunga,     [Imepokewa na Bukhari Muslim]

Mtume ﷺ akawaambiia [sisi tuna haki kwa nabii musa kuwashinda nyinyi basi mtume akafuna na akatuamrisha ifungwe.]        [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na ni bora kufunga pamoja na tarehe 10 tarehe 9 ili kuwakhalifu mayahudi kwani hata mtume Muhammad ﷺ alifunga miaka 9 aliyoishi madina siku ya Ashura’a na Maswahaba walipo mwambia kuwa Mayahudi waitukuza siku hii akasema:

“لئن بقيت إلى قابل لأصومن التاسع”

[Nikiisha mpaka mwakani nitafunga siku ya 9″]   Lakini mtume hakuishi.

[Imepokewa na Muslim na Abuu Daud.]

Na imekuja katika hadithi nyingine ya kutilia mkazo la hili la kuwakhalifu Mayahudi.

[صوموا يوم عاشوراء، وخالفوا فيه اليهود، صوموا قبله يوماً، أو بعده يوماً]    أخرجه أحمد وإبن خريمة والبيهقي

[fungeni siku ya Ashuura’a na muwakhalifu Mayahudi, fungeni siku kabla yake, au siku baada yake.]      [Imepokewa na Ahmad na Ibnu Khuzaymah na Al-Bayhaqiy.]

FADHLA YA KUFUNGA SIKU HII

Na katika kufunga siku hii kuna fadhla nyingi.

kwanza: ni kufwata sunna ya mtume Muhammad ﷺ.

Pili: imekuja katika hadithi ya mtume kwamba amesema:

عن أبي قتادة رضي اللَّه عنه ، أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ” صيام يوم عاشوراء، أحتسب على اللَّه أن يكفر السنة التي قبله    أخرجه مسلم وأبوداود

Kutoka kwa Abii Qatada radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume ﷺ amesema: [kufunga siku ya ashura’a natarji kwa ALLAH kwamba inafuta madhambi ya mwaka uliyopita]       [Imepokewa na Muslim na Abuu Daud.

Na madhambi yanayosamehewa ni madhambi madogo,ama madhambi makubwa ni lazima mtu alete Tawba kwa Allah.

Na hii ni fadhla kubwa kutoka kwa ALLAH.

UTARATIBU WA KUFUNGA SIKU YA ASHURA’A

Na kufunga swaum ya (Ashura’a) iko aina tatu.

1- kufunga tarehe kumi peke yake yaani (Ashura’a)

2- kufunga tarehe 9 na 10

3- kufunga tarehe 9,10,11 Zote hizi ni sahihi.

Na ubora katika aina hizo tatu ni kufunga 9,10,11,kama walivyo elezeya wanachuoni.

Imeadnikwa na

Fadhil Muhammad Shirazy

Mombasa –Kenya.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.