0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HUKUMU YA SWALA YA JAMAA

SOMO LA FIQHI

HUKMU YA SWALA YA JAMAA

Sheria imeamrisha Swala ya jamaa kwa wanaume wanaoweza na imemuonya mwenye kuiwacha. Na Mtume ﷺ alidhamiria kuwachoma wale wasioihudhuria. Alafu Mtume hakumruhusu kipofu kuacha jamaa, na dalili ya hilo ni: ya

1. Neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka kuhusu Swalah ya Hofu:

{وَإِذَا كُنتَ فِيهِمْ فَأَقَمْتَ لَهُمُ الصَّلَاةَ فَلْتَقُمْ طَائِفَةٌ مِّنْهُم مَّعَكَ}   النساء:102

[Na ukiwa na wao na ukawasimamishia Swala, basi na lisimame jopo miongoni mwao..] [4: 102]

Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hapa Ameamrisha kusimamisha jamaa katika hali ya hofu ya kivita na safari, basi katika hali ya amani na ukazi ni aula zaidi.

2. Hadithi iliyopokewa na Abu Hurarah Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume  alisema:

إِنَّ أَثْقَلَ صَلَاةٍ عَلَى الْمُنَافِقِينَ صَلَاةُ الْعِشَاءِ وَصَلَاةُ الْفَجْرِ، وَلَوْ يَعْلَمُونَ مَا فِيهِمَا لَأَتَوْهُمَا وَلَوْ حَبْوًا وَلَقَدْ هَمَمْتُ أَنْ آمُرَ بِالصَّلَاةِ فَتُقَامَ ثُمَّ آمُرَ رَجُلًا فَيُصَلِّيَ بِالنَّاسِ ثُمَّ أَنْطَلِقَ مَعِي بِرِجَالٍ مَعَهُمْ حُزَمٌ مِنْ حَطَبٍ إِلَى قَوْمٍ لَا يَشْهَدُونَ الصَّلَاةَ فَأُحَرِّقَ عَلَيْهِمْ بُيُوتَهُمْ بِالنَّارِ     رواه البخاري ومسلم

[Swala nzito zaidi kwa wanafiki ni Swala ya Isha na Swala ya Alfajiri. Na lau wao walijua Yaliyomo kwenye Swala mbili hizo, wangaliziendea japo kwa kujikokota na mimi nilidhamiria kutoa amri Swala kukimiwa, kisha nimuamrishe mtu awaswalishe watu, kisha nitoke na watu wakia  matita ya kuni niwaendee wale watu wasiohudhuria Swala niwachomee nyumba zao kwa moto]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Na Mtume ﷺ hadhamirii kuwachoma wale wasiohudhuria jamaa isipokuwa hiyo jamaa ni wajibu. Pia hawasifiwi wale wanaoacha kuhudhuria kwa unafiki, isipokuwa ni kwa uajibu wake.

3. Hadithii ya kipofu aliyemtaka ruhusa Mtume ﷺ aswali nyumbani kwake – na hana mtu wa kumuongoza njia-, na Mtume ﷺ akamwambia:

[هَلْ تَسْمَعُ النِّدَاءَ بِالصَّلَاةِ ؟] قَالَ : نَعَمْ ، قَالَ : [ فَأَجِبْ ] .   رواه مسلم

[Je unasikia mwito wa Swala?]  Akasema: ”Ndio”. Akasema: [Basi itikia]   [Imepokewa na Muslim.].

4. Hadithi iliyothubutu kutoka kwa Ibnu Mas’ud Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba yeye alisema:

مَنْ سَرَّهُ أَنْ يَلْقَى اللَّهَ غَداً مُسْلِماً ، فَلْيُحَافِظْ عَلَى هَؤُلاَءِ الصَّلَوَاتِ _ المكتوبة _ حَيْثُ يُنَادَى بِهِنَّ ، فَإِنَّ اللَّهَ شَرَعَ لِنَبِيِّكُمْ صلى الله عليه وسلم سُنَنَ الْهُدَى ، وَإِنَّهُنَّ مِنْ سُنَنِ الْهُدَى ، وَلَوْ أَنَّكُمْ صَلَّيْتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ كَمَا يُصَلِّي هَذَا الْمُتَخَلِّفُ فِي بَيْتِهِ ، لَتَرَكْتُمْ سُنَّةَ نَبِيِّكُمْ ، وَلَوْ تَرَكْتُمْ سُنَّةَ نَبِيِّكُمْ لَضَلَلْتُمْ ، وَمَا مِنْ رَجُلٍ يَتَطَهَّرُ فَيُحْسِنُ الطُّهُورَ ثُمَّ يَعْمِدُ إِلَى مَسْجِدٍ مِنْ هَذِهِ الْمَسَاجِدِ إِلاَّ كَتَبَ اللَّهُ لَهُ بِكُلِّ خَطْوَةٍ يَخْطُوهَا حَسَنَةً ، وَيَرْفَعُهُ بِهَا دَرَجَةً ، وَيَحُطُّ عَنْهُ بِهَا سَيِّئَةً ، وَلَقَدْ رَأَيْتُنَا وَمَا يَتَخَلَّفُ عَنْهَا _ أي صلاة الجماعة _ إِلاَّ مُنَافِقٌ مَعْلُومُ النِّفَاقِ ، وَلَقَدْ كَانَ الرَّجُلُ يُؤْتَى بِهِ يُهَادَى بَيْنَ الرَّجُلَيْنِ حَتَّى يُقَامَ فِي الصَّفِّ ”      رواه مسلم

[Mwenye kufurahika kukutana na Mwenyezi Mungu Kesho hali ya kuwa ni Muislamu, basi ajilazimishe na hizi Swala. Kwani zitatangwazwa. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Amemfaradhia Nabii wenu ﷺ nyendo za uongofu, na hakika hizi Swala ni miongoni mwa nyendo za uongofu. Na lau nyinyi mkiswali kwenye nyumba zenu kama anavyoswali nyumbani kwake huyu asiyehudhuria mgaliacha mwendo wa Nabii wenu, na lau mnaacha mwendo wa Nabii wenu mgalipotea. Na hakuna mtu yoyote anayejitwahirisha vizuri Kisha akaukusudia Msikiti mmoja kati ya hii Misikiti isipokuwa Mwenyezi Mungu Atamuandikia, kwa kila hatua anayoipiga, jema moja, Anampandisha daraja moja na Anampomoshea dhambi moja. Hakika niliona vile tulivyokuwa hakuna anayeacha kuihudhuria jamaa isipokuwa mnafiki anayejulikana unafiki wake. Na alikuwa mtu akiletwa na huku ameshikiliwa baina ya watu wawili- yaani akijishikiliza na wao- mpaka akasimamishwa kwenye safu]     [ Imepokewa na Muslim.].

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.