0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HEKIMA YA SWALA YA JAMAA NA FADHLA ZAKE

SOMO LA FIQHI

HEKIMA YA SWALA YA JAMAA NA FADHLA ZAKE

1. Kujuana kwa ndugu na wanaopendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wao kwa wao na kutilia nguvu ushikano wa mapenzi baina yao, mambo ambayo imani haiwi isipokuwa kwa hayo. Kwani hakuna njia ya Imani wala ya Peponi isipokuwa kwa kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.

2. Kuepukana mja na unafiki na Moto kwa aliyewahi takbiri ya kufungia Swala siku arubaini mfululizo, kwa hadithi aliyoipokea Anas Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume :

مَنْ صَلَّى لِلَّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا فِي جَمَاعَةٍ يُدْرِكُ التَّكْبِيرَةَ الْأُولَى كُتِبَتْ لَهُ بَرَاءَتَانِ بَرَاءَةٌ مِنْ النَّارِ وَبَرَاءَةٌ مِنْ النِّفَاقِ]    رواه الترمذي]

[Mwenye kuswali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu siku arubaini kwa jamaa, akawa anawahi takbiri ya kwanza, ataandikiwa kuwa mbali na Moto na kuwa mbali na unafiki]                 [Imepokewa na Tirmidhi.].

3. Kukusanyika Waislamu walio huku na kule na kuzizoweza Nyoyo zao kheri na utengefu.

4. Kushikamana Waislamu na kusaidiana kwao baina yao.

5. Kudhihirisha Ibada za Dini na nguvu yake.

6. Kuziunganisha nyoyo za Waislamu, kwa kumfanya mweupe na mweusi, Mwarabu na asiyekuwa Mwarabu, mkuu na mdogo, tajiri na masikini, wote wakawa pamoja ndani ya msikiti mmoja, nyuma ya Imamu mmoja na katika wakati mmoja, wote wanaekelea kibla kimoja na muelekeo mmoja.

7. kuwatia hasira maadui wa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Waislamu bado wana nguvu iwapo wataendelea kutunza utekelezaji Swala misikitini.

8. Kufutiwa dhambi na kupandishwa daraja. Imepokewa na Abu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema:

أَلا أَدُلُّكُمْ عَلى مَا يمْحُو اللَّهُ بِهِ الخَطَايَا، وَيَرْفَعُ بِهِ الدَّرَجَاتِ؟ قَالُوا: بَلى يَا رسولَ اللَّهِ. قَالَ: إِسْباغُ الْوُضُوءِ عَلى المَكَارِهِ، وَكَثْرَةُ الخطى إِلى المَسَاجِدِ، وَانْتِظَارُ الصَّلاةِ بعْد الصَّلاةِ، فَذلِكُمُ الرِّباطُ، فَذلكُمُ الرِّباطُ     رواه مسلم

[Je si niwajulishe kitu kinacho sababisha kufutiwa dhambi na Mwenyezi Mungu na kupandishwa daraja? Wakasema: “Kwani? Tujulishe ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu” Akasema: “Nikueneza maji ya kutawadhia kwenye viungo, na kuwa na hatua nyingi za kwenda msikitini, na kungoja Swala baada ya Swala. Kwani huko ndiko kujitolea katika kusimamisha Dini]       [Imepokewa na Muslim.].

9. Swala ya jamaa ni bora kuliko Swala ya mwenye kuswali peke yake kwa daraja ishirini na saba. Ibnu ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake amepokewa kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alisema:

 [صلاة الجماعة أفضل من صلاة الفذ بسبع وعشرين درجة ]   رواه البخاري ومسلم 

[Swala ya jamaa ni bora kuliko Swalah ya mwenye kuswali peke yake kwa daraja ishirini na saba]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.