SOMO LA FIQHI
Suali: Ni ipi hukmu ya mwenye kuacha swala?
Jawabu: Hukumu ya mwenye kuacha Swala inategemea na namna anvyo itakidi juu ya swala na hii inakuwa ni hali mbili:
Hali ya kwanza: Mwenye kuacha Swala kwa kukanusha uwajibu wake:
Hali hii kwanza Atafahamishwa uwajibu wa Swala akiwa hajui. Na Akiendelea kukanusha, basi yeye atakuwa kafiri, mkanushaji wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na umoja wa Waislamu.
Hali ya pili: Mwenye kuacha Swala kwa uvivu:
Na kwa hali hii wanachuoni wamekhatalifiana juu Kauli mbili:
Kauli ya kwanza: Mwenye kuacha Swala kwa uvuvi atakuwa ni Faasiq wala hakufuru na kutoka katika Uislamu, na msimamo ni ndio msimamo wa wengi katika wanachuoni.
Na dalili walizo zitegemea ni neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:
{إِنَّ اللَّهَ لا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ} النساء:47
[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye] [Al-Nnisaa:47]
Wanasema mwenye kuacha Swala atakuwa ameingia katika aya hii madamu hakuwa ni mwenye kumshirikisha mwenyezi Mungu
Na katika Hadithi wametolea dalili hadithi hii:
حديث عتبان بن مالك رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: [إن الله حرم على النار من قال لا إله إلا الله، يبتغي بذلك وجه الله] رواه البخاري
Amepokea Utbaan bin Maalik radhi za Allah ziwe juu yake Kwamba Mtume Amesema [Hakika Mwenyezi Mungu amemuharimishia moto Mwenye kusema hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu akitaka kwa hilo uso wa Mwenyezi mungu.] [Imepokelewa na Bukhari]
Kauli ya pili: Mwenye kuacha Swala kwa kukusudia na uvivu atakuwa amekufuru. Na ni juu ya kiongozi amlinganie kuswali na amuorodheshee toba kwa muda wa siku tatu. Basi akitubia ni sawa, na akitotubia atamuua kwa kuwa ameritadi.
Na wametegemea neno lake Mwenyezi Mungu aliposema:
{فَإِنْ تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ} التوبة:11
[Basi wakitubu na wakashika Sala na wakatoa Zaka, basi ni ndugu zenu katika Dini.] [Al-Tawba:11]
Wakasema aya inamanisha kuwa mtu asie swali si ndugu yenu katika Dini.
Na kwa kauli yake Mtume ﷺ:
[العهد الذي بيننا وبينهم الصلاة، فمن تركها فقد كفر] رواه أحمد والترمذي
[Ahadi iliyoko baina ya sisi na wao ni Swala. Yoyote yule atakayeiacha basi atakuwa amekufuru]
[Imepokewa na Tirmidhi.]
Na kauli yake ﷺ:
[بين الرجل وبين الشرك والكفر ترك الصلاة]
[Hakika baina ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha Swala] [Imepokewa na Muslim.]
Na huu ndio msimamo ulio Mash’hri wa Madhhebu ya Imam Ahmad.na ndio kauli ya Sheikhul Islam Ibnu Taymiyah na Sheikh Ibnu baaz na Sheikh Ibnu Uthaymin kwa yule aliacha swala kabisa ama kwa yule anae swali na kuacha huyu hakufuru.