0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

FADHLA ZA SWALA

SOMO LA FIQHI

Suali: Ni zipi Fadhla za Swala?

Jawabu: Swala ina Fadhla nyingi Miongoni mwa fadhla zake ni hizi:

1. Swala ni nuru kwa mwenye kuswali. Mtume ﷺ amesema:

[ والصلاة نور]       رواه مسلم

[Na Swala ni Nuru]       [ Imepokewa na Muslim.].

2. Swala ni kafara ya dhambi. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema:

{وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ}       هود:114

[Na simamisha Swala ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zinazokaribiana na mchana. Hakika mema yanafuta maovu. Hayo ni makumbusho kwa wenye kukumbuka]      [11: 114].

Na amesema Mtume :

رَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ، هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ؟  ، قَالُوا: لَا يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ، قَالَ:  فَذَلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، يَمْحُو اللهُ بِهِنَّ الْخَطَايَا      رواه البخاري ومسلم

[Mnaonaje, lau kuna mto mlangoni mwa mmoja wenu ambao anaoga ndani yake kila siku mara tano, je kutasalia chochote cha uchafu mwilini mwakeWakasema: Hakutasalia uchafu wowote katika mwili wake. Akasema Mtume ﷺ: Huo ndio mfano wa Swala tano,. Mwenyezi Mungu kwa hizo Swala anayafuta madhambi]   [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

3. Swala ni sababu ya mtu kuingia Peponi. Mtume ﷺ alimwambia Rabi’ah bin Ka’ab, alipomtaka wasuhubiane naye Peponi,: Mtume akamjibu:

    [ فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ ، بِكَثْرَةِ السُّجُودِ ]     رواه مسلم

[Nisaidie kwa kuishughulisha nafsi yako kwa kusujudu sana]     [Imepokewa na Muslim.].



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.