HII NISHAHADA YA KUMUINGIZA MTU PEPONI AMA MATONI ?
Sote tunajua kuwa mtu anapo taka kusilimu nilazima kwanza apige shahada mbili,nao ni kusema
Ash’hadu an laailaha illa Allah,Wa’ash’hadu anna Muhamadan Rasulullah.
Nakuiri kwa myo na kubaini kwa ulimi ya kuwa hapana mola apase kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi mungu na kuwa Mtume Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Na mtu anapo piga shahada huwa ashakuwa Muislamu,na haya ndio Mafundisho tulio funzwa na Qur’ani na Sunna za bwana mtume Muhamad Rehma na amani zimfikie yeye.
Asema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.
{شَهِدَ اللَّهُ أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ}
آل عمران:18
[Mwenyezi Mungu, na Malaika, na wenye ilimu, wameshuhudia kuwa hakika hapana mungu ila Yeye, ndiye Mwenye kusimamisha uadilifu; hapana mungu ila Yeye Mwenye nguvu na Mwenye hikima.]
[Al-Imraan:18]
Na katika Hadithi Mtume ﷺ amesema:
[أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى : يَشْهَدُوا أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللَّهِ] رواه البخاري ومسلم
[Nimeamrishwa nipigane na watu Mpaka washuhudie yakuwa hapana Mola apase kuabudiwa kwa haki ila MwenyeziMungu na kuwa Muhamad ni mtume wa Mungu.] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Na Mtume ﷺ alipo mpeleka swahaba wake Muaadh Radhi za allah ziwe juu yake Yamen alimwamrisha kwanza awalinganie watu katika Tawhiid Kumuamini mungu mmoja na mtume wake. na mtu akishuhudia hivyo huwa ashakuwa muislamu.
Lakini la ajabu na kushangaza ni kwa hawa Mashia hilo halimtoshi mtu kuwa Muislamu mpaka
ashuhudie na mashahada mengine ili awe Muislamu.
Ushudie kuwa Abubakr na Umar na Uthman Bibi Aisha kuwa ni watu wa Motoni.
Na ushuhudie kuwa Sayyidna Ali radhi za allah ziwe juu yake ni walii wa mungu na Bibi Fatima na watoto wake ni wasii wa Allah.
Ajabu kubwa sana, yaani ukitaka kuwa Muislamu mpaka ushudie yakuwa bibi zake Mtume ni watu wa motoni,na Maswahaba wake watukuf walio itetea hii dini kwa hali na mali,pia ushuhudie kuwa ni watu wamotoni. Subhanallah!
Ndio tukauliza Hizi ni shahada za kumuingiza mtu motoni ama peponi?
Na hili japo kuwa hawakuandika kwenye vitabu vyao kwa sababu ya (Taqqiya) lakini kwa sasa mashekhe wao wabainisha wazi katika mafunzo yao na wanapotaka kumuingiza mtu kwenye Ushia. japo kuwa Masheikhe wakishia walioko Africa hawajakuwa na ujasiri wa hilo.
Tazama huyu hapa sheikh wakishia akimtemsha Shahada alietaka kuwa Mshia.