0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

HAWA NI MIUNGU AMA NI MAIMAMU?

HAWA NI MIUNGU AMA NI MAIMAMU?

Mwenyzi Mungu aliyetukuka ndie peke yake Mwenye sifa za ukamilifu na ndie mumba mbingu na aradhi na viliomo

baina yake.Yeye peke ndie anaejua ilimu ya gheyb na hana mshirika na yoyoye katika umbaji wake wala kuabudiwa kwake.

Allah anasema katika kitabu chake kitukufu:

{قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ}   النمل: 65

[Sema: Hapana katika mbingu na ardhi ajuaye ya ghaibu isipo kuwa Mwenyezi Mungu.]     [Al-Naml:65]

Hata manabii walio tumilizwa wala Malaika walio karibu hawajui ilimu ya Gheyb ila kwa wale walifunuliwa na yeye Allah Subhnahu Wataala.

Asema Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

{عَالِمُ الْغَيْبِ فَلَا يُظْهِرُ عَلَى غَيْبِهِ أَحَدًا * إِلَّا مَنِ ارْتَضَى مِنْ رَسُولٍ}     الجن:26-27

“Yeye ndiye Mwenye kujua ya siri, wala hamdhihirishii yeyote siri yake Isipo kuwa Mtume wake aliye mridhia.”

Lakini la ajabu na Kushangaza ni kwa itikadi za hawa Mashia wanodai Uislamu.Hebu tuangalia namna wanavyo

itakidi kwa Maimamu wao kwa mujibu wa vitabu vyao wanavyo vitegemea.

Maimu wajua ilimu ya Gheyb.

Yamekuja katika kiabu chao wanacho kiegemea zaidi [Al-Kaafiy]

قال أبو عبد الله ” إني لأعلم ما في السماوات وما في الأرض وأعلم ما في الجنة والنار وأعلم ما كان وما يكون” (الكافي 1/204 (

Amesema Abuu Abdillah ” hakika yangu mimi najua yaliyomo mbinguni na yaliyomo Ardhini na ninajua yaliyomo

Peponi na Motoni na ninajua yaliokuwa na yatakao kuwa.”  Al-Kaafiy   1/204

Wanauwezo wakufisha na kuhuisha.

Kama yalivyo kuja kwenye kitabu chao “Bihaarul- Anwaar”  

وقال سلمان -كما يفترون-: “لو أقسم أبو الحسن على الله أن يحيي الأوّلين والآخرين لأحياهم” [بحار الأنوار: 41/201، الخرائج والجرائح ص82]

Na Amesema Salmaan ” lau angeapa babayake Hassan juu ya Mwenyezi Mungu amfufulie wa mwanzo na wamwisho

basi Mungu angewahuisha.

[Bihaarul-Anwaar 41/204 na kitabu cha Al-Kharaaij wal-Jaraaih uk.82

Na waitakidi kuwa Maimu wanajua siku ya kufa kwao na Imamu asiejua hayo basi huyo hajakuwa Imamu wa kweli.

Ndio tukauliza hawa ni Maimamu ama ni Miungu?

Ndio utaona Mashia badala ya Kumuaomba Mungu wanapo kuwa na shida  wao huwaomba Maimamu wao,Badala

 ya kusema Yaa ALLAH, Yaa Rahmaan wao husema Yaa ALI.Yaa Husein.


Msikile Mmoja katika Mashekhe wao vile anavyo sema Kuhusu Maimu wao

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.