0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUINGIA PEPONI AU KUMLILIA HUSEIN RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE??

PEPO  AU KUMLILIA HUSEIN RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAKE?? 

Kuingia peponi ndio matakwa ya kila muislamu na muimin,kwa sabubu pepo ndio bidhaa ilio ghali kama alivyo sema mtume wa Mwenyezi Mungu,na waumini walipo acha starehe za dunia na kufanya ibada kwa wingi lengo ni kutaka Radhi za Mungu na Mwishowe waingizwe peponi.

Kama mwenyezi Mungu alaiyetukuka aliyo sema kwenye kitabu chake kitukufu:

إِنَّ اللَّهَ اشْتَرَىٰ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ أَنفُسَهُمْ وَأَمْوَالَهُم بِأَنَّ لَهُمُ الْجَنَّةَ ۚ يُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَيَقْتُلُونَ وَيُقْتَلُونَ ۖ وَعْدًا عَلَيْهِ حَقًّا فِي التَّوْرَاةِ وَالْإِنجِيلِ وَالْقُرْآنِ ۚ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ مِنَ اللَّهِ ۚ فَاسْتَبْشِرُوا بِبَيْعِكُمُ الَّذِي بَايَعْتُم بِهِ ۚ وَذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ.   التوبة:111

[Hakika Mwenyezi Mungu amenunua kwa Waumini nafsi zao na mali zao kwa kuwa wao watapata Pepo. Wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu – wanauwa na wanauwawa. Hii ni ahadi aliyo jilazimisha kwa Haki katika Taurati na Injili na Qur’ani. Na nani atimizae ahadi kuliko Mwenyezi Mungu? Basi furahini kwa biashara yenu mliyo fanya naye. Na huko ndiko kufuzu kukubwa,]      [Tawba:111

Kwa sababu hiyo ndio utona Waumini wako teyari kujitolea kwa lolote lile kwa ajili ya kupata radhi za Mungu pepo.

Na Mwenyezi Mungu yeye ndie aliesema kuwa atakae epushwa na moto na kuingizwa peponi huyo ndie aliefaulu.

فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ}     آل عمران:185}

“Na atakaye epushwa na Moto na akatiwa Peponi basi huyo amefuzu”    [Al-Imraan:185]

Na vile vile Manabi na watu Wema walikuwa wakimuomba Mwenyezi Mungu awaingize kwenye pepo yake,na kila Muislamu matarajio yake ataka aingie peponi na awe ni katika watakao ambiwa:

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ }   النحل:32}

[Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema, wanawaambia:Amani iwe juu yenu! Ingieni Peponi kwa sababu ya yale mliyo kuwa mkiyatenda.]     [Al-Nnahl:32]

Laikini la ajabu na lakushangaza ni kwa hawa Mashia pepo kwao silo lamuhimu sana,lamuhimu kwao ni kumlilia Sayyidnal Husein,wako radhi lau watakhiyarishwa wakifa waingie peponi au wakae duniani kwa ajili ya kumlilia husein watakhiyari kubaki dunani ili wapatai kumlilia Husein kama hili la kulia ndilo lengo kubwa la huyu Mwanadamu.

                 MSIKILIZE MWANACHUONI WAO ANAVYOSEMA

Labda mtu huweza akajadili kuwa huo sio msimamo wa mashia wote,ni kweli huenda ikawa ni hivyo lakini mbona hatupati mwanachuoni wa kishia alie mrudi na kumpinga kuwa si sawa ?

Mashia hili la kumlilia Husein kwao limekuwa ni ibaada kubwa, kama kwamba dini imeamrisha kufanya hivyo haliyakuwa dini limekataza watu kuomboleza katika Msiba amesema Mtume rehma na amani zifikie yeye sikatika sisi atakae jipiga matafu,na kupasuwa mifuko (nguo) na kuomba maombi ya kijahiliya.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.