SOMO LA FIQHI
Suali: Ni zipi Fadhla za Swala?
Jawabu: Swala ina Fadhla nyingi Miongoni mwa fadhla zake ni hizi:
1. Swala ni nuru kwa mwenye kuswali. Mtume ﷺ amesema:
[ والصلاة نور] رواه مسلم
[Na Swala ni Nuru] [ Imepokewa na Muslim.].
2. Swala ni kafara ya dhambi. Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Amesema:
{وَأَقِمِ الصَّلَاةَ طَرَفَيِ النَّهَارِ وَزُلَفًا مِّنَ اللَّيْلِ ۚ إِنَّ الْحَسَنَاتِ يُذْهِبْنَ السَّيِّئَاتِ ۚ ذَٰلِكَ ذِكْرَىٰ لِلذَّاكِرِينَ} هود:114
[Na simamisha Swala ncha mbili za mchana na nyakati za usiku zinazokaribiana na mchana. Hakika mema yanafuta maovu. Hayo ni makumbusho kwa wenye kukumbuka] [11: 114].
Na amesema Mtume ﷺ:
رَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهْرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ مِنْهُ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسَ مَرَّاتٍ، هَلْ يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ؟ ، قَالُوا: لَا يَبْقَى مِنْ دَرَنِهِ شَيْءٌ، قَالَ: فَذَلِكَ مَثَلُ الصَّلَوَاتِ الْخَمْسِ، يَمْحُو اللهُ بِهِنَّ الْخَطَايَا رواه البخاري ومسلم
[Mnaonaje, lau kuna mto mlangoni mwa mmoja wenu ambao anaoga ndani yake kila siku mara tano, je kutasalia chochote cha uchafu mwilini mwakeWakasema: Hakutasalia uchafu wowote katika mwili wake. Akasema Mtume ﷺ: Huo ndio mfano wa Swala tano,. Mwenyezi Mungu kwa hizo Swala anayafuta madhambi] [ Imepokewa na Bukhari na Muslim.].
3. Swala ni sababu ya mtu kuingia Peponi. Mtume ﷺ alimwambia Rabi’ah bin Ka’ab, alipomtaka wasuhubiane naye Peponi,: Mtume akamjibu:
[ فَأَعِنِّي عَلَى نَفْسِكَ ، بِكَثْرَةِ السُّجُودِ ] رواه مسلم
[Nisaidie kwa kuishughulisha nafsi yako kwa kusujudu sana] [Imepokewa na Muslim.].