CHOZI LITAKUINGIZA PEPONI MIAKA !!
Kulia anapopatikana na msimba si dhambi wala si haramu kwa sababu hili ni maumbile ya mwanadamu kufurahi na kucheka anapopata furaha huwa analia na kuhuzunika anapopatwa na msimba.
Ila tu sharia imeweka makatazo watu wasivuke mipaka wakati wa kufurahi kwa kufanya Mambo yaliyo haramishwa na kumuasi Mwenyezi mungu na vile vile wakati wa huzuni kwa kumsahu Mungu na kusema yasiofaa. Bali muislamu atakikana awe ni mwenye kuchunga mipaka ya Mungu kwa hali zote mbili furaha na msimba.
Amesema Mtume Rehma na amani zimfikie yeye:
عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال { ليس منا من ضرب الخدود ، وشق الجيوب ، ودعا بدعوى الجاهلية رواه البخاري ومسلم
Kutoka kwa Abdillah bin Mas’uud Radhi za Allah ziwe juu yake kutoka Mtume Rehma na amani zimfikie yeye Amesema: [si katika sisi atakae jipiga Matavu (wakati anapo patikana na Msiba) na kupasua Mivuko (nguo) na kuita miito ya kijahiliya] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Na dini yetu si dini inayopenda misiba na kuwa watu wawe ni wenye kukaa na kujitia huzuni kila wakati. Ndio pale sheria ikaruhusu watu waliofiliwa wakae siku tatu wala wasizidishe na hizi siku tatu ni kwa wale watu wa nyumbani waliofiliwa ili wapate kutaazi kwa wale watu wanaoishi mbali.
Lakini kwa dini ya Mashia hili la kuomboleza kwao ndio dini. Utawaona daima wako Makaburini waomboleza na kulia na utakuta bid’aa zote zinazo ambatana na kifo na tanzia utakuta zimetoka kwao.
Na isitishe wameweka mlango Makhsusi wa watu kumililia sayyidnal Husein na wameweka hadithi chungu mzima kwa fadhla za kumlilia sayyidal Hussein radhi za Allah ziwe juu yake.
Miongini mwa hadithi za uzushi na hadithi hizi.
قال الصادق (ع) : ” من ذَكَرنا أو ذُكرنا عنده فخرج من عينه دمعٌ مثل جناح بعوضة ، غفر الله له ذنوبه ولو كانت مثل زبد البحر “. أمالي الصدوق مجلس 17 رقم4 ص 278
Amesema Al-Swaadiq (A.S.) “Mwenye kutukumbuka au tukatajwa mbele yake yakatoka kwenye macho yake chizi mfano wa umbu, basi Mwenyzi Mungu atamsamehe dhambi zake japo kuwa dhambi zake ni kama povu la baharini.”
[Amaali Swaduuq kikao cha 17 namba 4 ukurasa 278]
Na katika hadithi nyingine za uzushi ni hadithi hii.
كان علي بن الحسين (ع) يقول : ” أيمّا مؤمن دمعت عيناه لقتل الحسين بن علي دمعة حتى تسيل على خدّه ، بوّأه الله بها في الجنة غرفا يسكنها أحقابا” أمالي الطوسي ص34
Alikuwa Ali ibnul –Husein (A.S.) Akisema: “Muumin yoyote macho yake alitokwa na machozi kwa kifo cha Husein bin Ali chozi lililo tiririka kwenye tavu lake mwenyezi mungu atamuandalia kwa chozi hilo ghorofa katika pepo aishi humo milelele” [ Amaali Al-Tuusiy ukurasa 34].
Na kutoka na Hadithi hizi walizo wasingizia maimamu wao ndo utaona majabu na vituko juu hili,mtu atafuta kujiliza kwa namna yoyote ile hata kama hana kilio.
Na utaona siku ya Ashuraa wameibadilisha kuwa ni siku ya huzuni kila mwaka kutoka mabarabarani na kujipiga mapanga na visu wakihuzunika kwa kifo cha Husein,kisha utasikia arbainiyatul Husein na kadhalika.
Mtazame huyo Sheikh wao,hiko ni kicheko ama nikilio?