الحديث الحادي والثلاثون
“ازهد في الدنيا يحبك الله”
عَنْ أَبِي العَبّاسِ سَهلِ بْن سَعْدٍ السّاعِدِيِّ رضي الله عنه قَالَ : جَاءَ رَجُلُ إِلى النَبِي صلى الله عليه وسلم فَقَالَ : يَا رَسُولَ اللَّهِ دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ أَحَبَّنِي اللَّهُ وَأَحَبَّنِي النَّاسُ . فَقَالَ: [ازْهَدْ فِي الدُّنْيَا يُحِبُّكَ اللَّهُ وَازْهَدْ فِيمَا عِنْدَ النَّاسِ يُحِبُّكَ النّاسُ]
رَوَاهُ ابْنُ مَاجَهْ وَغَيْرُهُ بِأَسَانِيدَ حَسَنَةٍ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ مُحَمّد بن صَالِح العُثَيْمِين رحمه الله تعالى
HADITHI YA 31
UPE ULIMWENGU KISOGO ALLAAH ATAKUPENDA
Kutoka kwa Abu Al-‘Abbaas Sahl bin Sa’ad As-Saa’idiy Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye alisema:
Mtu alikuja kwa Mtume ﷺ na akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyeezi Mungu, nielekeze kitendo ambacho nikitenda Mwenyezi Mungu atanipenda na watu watanipenda. Akasema ﷺ : [Upe ulimwengu kisogo Mwenyeezi Mungu atakupenda, na jiepushe na vilioko Mikononi mwa watu na watu watakupenda.]
[Imepokelewa na Ibn Maajah na wengineo kwa mtiririko mzuri wa mapokezi.]