0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

AMINAH ASSILMI

HISTORIA YA MAMA AMINAH ASSILMI

Waliosilimu wanazo changamoto nyingi na zinazotishia, hivi kwamba asiye na imani kamili aweza kuteteleka na kurudi nyuma.

Lakini wale waliojaaliwa na Allah [swt] husimama kidete na historia zao twazisoma hata leo, nakila zikisomwa sisi hupata mafunzo ya subira katika yanayotusibu kama vile Sahaba mtukufu na Muadhin wa Mtume [saw], Seyyidna Bilal [ra], kadiri mateso yalivyozidi alikisema ‘Ahad, Ahad,Ahad’.

Katika miaka yetu hii tunao watu walioonyesha misimamo imara licha a mateso waliokuwa wakipitia, mfano ni mama Aminah Asilmi aliyezaliwa Oklahoma, Amerika na kubatizwa katika kanisa la Southern Baptist.

Alifuzu katika chuo na shahada ya uanahabari, haswa utangazaji wa TV, na akajitokeza kama mtetezi wa haki za wanawake, aliupinga Uislam eti unawanyanyasa wanawake, alitaka uhuru wa mavazi, pamoja na kuhoji kwa nini katika Uislam wanawake hawaruhusiwi kuolewa na mume zaidi ya mmoja hali waume wameruhusiwa kuoa mke zaidi ya mmoja.

Historia ya kusilimu kwake inaanza pale kosa la kitarakilishi, akasajiliwa katika kitengo cha michezo ya kuigiza ya TV, japo kuwa mwenyewe hakutaka kuingia katika kitengo hicho, lakini uwepo wa wanafunzi wenzake watatu Waislam, naye akiwa mkereketwa wa ukristu akaona abakie katika kitengo hicho ili awakaribishe hao Waislamu katika ukristu.

Alitumia mbinu ya zamani ya wakristu eti ‘ Yesu anawapenda Waislam na alikufa kwa ajili ya kuwaokoa na dhambi zao’
Mwenyewe aliona ajabu kuwa alitaka kuwatoa Waislamu katika Dini yao, lakini mwishowe akawa ni mwenye kusilimu!, Baada ya kukumbana na Waislam kwa mara ya kwanza, alianza kutafiti kwa miaka miwili lengo ni yeye apate wepesi wa kuwaleta waislamu kwa ukristu. Katika kipindi hichi aliisoma Quraan tafsiri yote na hoja alizozipata alikubaliana kabisa na Imani na Dini ya Kiislamu, na akaamua kusilimu kwa khiari yake tarehe 21/5/1977, akaanza kuvaa mavazi ya sitara pamoja na kufuata yote aliyokuwa akipinga.

Tendo hili la Kusilimu kwake lilimfanya apoteze marafiki wake aliokuwa akishirikiana nao katika pati za kila weekend maana hakushiriki tena katika maasi yao. Dada yake aliyekuwa mtaalam wa akili alimuona kama aliyepoteza akili, naye Baba mzazi aliposikia binti yake amesilimu aliazimu kumwua kwa risasi, kwa kuwa aliona afadhali ‘awe amekufa’.

Mumewe, baba wa watoto wake wawili naye alimpa talaka, na kazini akatimuliwa eti kuvaa baadhi ya nguo kutawatishia watazamaji.

Alipo enda mahakamani ili adai haki yake ya kukaa na kuishi na wanawe, alinyimwa haki hiyo na jaji alimwambia achague baina ya mambo haya mawili:

1. Aukatae Uislamu apewe watoto au
2. Abakie Muislam na awasahau watoto.
Hebu fikiri kumzuia mzazi wa kike asiwakaribie watoto wake au kuwaona!, huku nyuma wakristo wakawa wanadai kuwa ni adhabu kwa kuuasi Ukristu, kwa hivyo watoto wakakabidhiwa mtalaka wake, alibakia na majonzi lakini akafanya subira ya hali ya juu. Alibakia na Uislamu wake na kuendelea kuwa mzuri kwa jamaa zake akiwaonyesha heshima ya Uislam, akajiepusha na matendo yote maovu, na ajabu Allah [swt] , wale walio kuwa maadui wakaanza kumkaribia, na wakwanza kuukubali Uislam ni nyanya yake mwenye umri wa miaka zaidi ya mia moja [100], kisha baadaye baba yake aliyetaka kumwua kwa kusilimu, kisha mama yake, dada yake aliyemuona kuwa wazimu kwa kusilimu kwake, mtalaka wake pia alisilimu na watoto wakasilimu walipo fikia umri wa miaka ishirini na moja [21]. Angalia neema ya Uislam!.

Aminah Asilmi hakumrudia mtalaka wake, bali aliolewa kisheria na mume mwingine na Allah akamjaalia mtoto wa kiume.

Twaweza kusema kila alichopoteza hapo mwanzo, Allah [swt] alimrudishia na kumpa kazi kubwa na ni ulinganizi kupitia shirika la International Union of Muslim Women.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.