0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MYAHOODI RABII YOUSEF COHEN

KUSILIMU KWA MYAHOODI RABII YOUSEF COHEN

Rabii Yousef Cohen alizaliwa Brooklyn, Amerika mwaka wa 1971, alikuwa mfuasi wa satmar, kikundi katika makundi ya kiyahoodi akiitwa Joseph Cohen. Alioa Lona Cohen myahood kama yeye na wakajaaliwa watoto wane.

Mwaka wa 1998, alisafiri Israeli na kuishi katika makaazi ya Ghosh Gatif, katika ukanda wa Gaza na baadaye akaghura kwenda Netivot kusini mwa Israeli. Rabii Yousef Cohen alikutan na Waislam kwa mara ya kwanza katika safari yake ya mara kwa mara katika soko la zamani huko Jerusalem, na akapewa kwa mara ya kwanza tafsir ya Quraan kwa lugha ya kiingereza.

Katika mahojiano na channel 10 TV alisema,
Nilipofunguwa Quran [tafsir] kwa mara ya kwanza, sikuweza kuiweka chini. Nikile nilikuwa
Naamini vile uyahoodi unatakiwa uwe. Kila kukosolewa kwa wayahood katika Quraan kulikuwa
Sawa na bila chuki. Bila shaka Allah akituonyesha wayahood, namna ya kujirudi wenyewe na
Kuirudia Haki [Uislam] ya Mwenyezi Mungu’

Baada ya utafiti wake, Rabii Yousef Cohen alimkabili mkewe Lona Cohen, mfuasi sugu wa uyahoodi akisema, nakupenda, na nataka kuwa mkweli kwako……… nimesoma Quraan, na nakubaliana na yote yaliyoko ndani yake, na nikiendelea mimi nina dini ya uyahoodi ntakuwa si mkweli’.

Baada ya mazungumzo hayo na mkewe, alisilimu na kupewa jina, Yousef Mohammad al Khattab, mkewe alishtuka mno, naye akaanza kutafiti kwa msaada wa mumewe,na baada ya majuma matatu, Lona Cohen pamoja na wanawe wanne wakasilimu na kuiacha dini ya uyahood.

Muda mchache walihama hadi Al-Toor magharibi mwa Jerusalem wanako ishi hata leo. Al-Khattab anafanya kazi katika shirika la Kiislam, na mno anawalingania wayahoodi waje katika Uislam.

Kitendo hichi cha kuwalingania wayahoodi Uislam kimemfanya achukiwe sana katika Israeli na kupendwa san asana na jamii ya Waislam.

Angalia kitabu
They are extremely smart or
Extremely ignorant


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.