0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MUHAMAD ALI CLAY

MUHAMAD ALI CLAY

Katika watu Mash’huri walio ongoka na kupata Nuru ya Uislamu ni Muhamad ali

Muhammad Ali alizaliwa mwaka 1942 katika mji wa Louisville, Kentucky, kwa familia maskini ya Wamarekani weusi  mnamo 17 Januari 1942 akijulikana kwa jina la Cassius Marcellus Clay

Alipata usumbufu yeye na  familia yake kutoka ubaguzi wa rangi ambayo ilikuwepo katika

kipindi hicho.

Alikuwa mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. Amepata kuwa bingwa wa uzito wa juu mara tatu.

Alisilimu mwaka 1975 na baada ya kusilimu na kujua dini ya haki alikwa na msimamo imara katika dini jambo lililo mpelekea kuhukumiwa badda ya kukataa kushiriki katika vita Vietnam mwaka 1967.

Alikamatwa na kupatikana na hatia juu ya rasimu ya ukwepaji mashtaka, wakamvua taji lake la uwanamasumbwi, na leseni yake ya uwanamasumbwi ikazuiliwa. Hakufungwa, lakini hakupambana kwa takriban miaka minne mpaka hapo rufaa yake ilipofanyiwa kazi na Mahakama Kuu ya Marekani, ambapo akaja kushinda.

Na alijulikana baada ya kusilimu kwake kuwa mtu mtulivu na kulingania amani duniani.

Hakuwa ni mwenye kujiona au kijangamba bali alikuwa akiona watu wote ni sawa mbele ya Mwenyezi Mungu.

Na mwaka 1972 alifunga safari ya kwenda Makkah kuhiji,na baade kuzuru sehemu kadha katika nchi ya Saudia na kulakiwa na wanachi na wakuu wa nchi hiyo.

Na baada ya kustafu katika mchezo wa ndondi alijihusisha katika kufanya matendo ya kusaidia wasio jiweza ,nchini America na sehemu mbali mbali duniani.na alipewa zawadi na umoja wa mataifa kwa juhudi yake katika kusaidia watu.

Na alichangia kujenga misikiti zaidi 170 nchini America na kusilimisha watu wengi.

Na walipotaka Hollywood kuwakirimu wasanii mbali mbali katika Los Angeles Januari ya mwaka 2002 alikataa kuwekwa nyota yake kwenye sakafu na watu kutembea juu yake kwa sababu ya kuhishimu jina la mtume Muhammad licha ya kuweko zaidi ya wasini 2500 ni mwana sanii peke jina lake limeandikwa kwenye ukuta wala halikuandikwa kwenye sakafu ya watu kutembelea.

Na kwa matokeo wa mchezo wa ndondi alipawa na   Ugonjwa wa Parkinson 1984  na alikuwa ni mwnye subira na alikuwa akisema Allah amenioja ili kumjulisha kuwa simkubwa bali yeye allah ndie mkubwa

Na tarehe 2/6/2016 alilazwa Phoenix Hospital katika wilaya ya Arizona baada ya kuzidiwa na maradhi na terehe 4/6/2016 alifariki Dunia akiwa na umri wa miaka 74.

Na kuzikwa katika mji wake aliozaliwa Jiji la Louisville.

Mungu amuweke pema pamoja na wema.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.