0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

041. Riyadhu Swalihina Mlango wa Subira Hadithi ya 17


BUSTANI YA WATU WEMA


رياض الصالحين


وعنْ أبي عبدِ اللَّهِ خَبَّابِ بْن الأَرتِّ رضيَ اللَّهُ عنه قال : شَكَوْنَا إِلَى رسولِ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم وَهُو مُتَوسِّدٌ بُردةً لَهُ في ظلِّ الْكَعْبةِ ، فَقُلْنَا : أَلا تَسْتَنْصرُ لَنَا أَلا تَدْعُو لَنَا ؟ فَقَالَ : « قَد كَانَ مَنْ قَبْلكُمْ يؤْخَذُ الرَّجُلُ فيُحْفَرُ لَهُ في الأَرْضِ في جْعلُ فِيهَا ، ثمَّ يُؤْتِى بالْمِنْشارِ فَيُوضَعُ علَى رَأْسِهِ فيُجعلُ نصْفَيْن ، ويُمْشطُ بِأَمْشاطِ الْحديدِ مَا دُونَ لَحْمِهِ وَعظْمِهِ ، ما يَصُدُّهُ ذلكَ عَنْ دِينِهِ ، واللَّه ليتِمنَّ اللَّهُ هَذا الأَمْر حتَّى يسِير الرَّاكِبُ مِنْ صنْعاءَ إِلَى حَضْرمْوتَ لا يخافُ إِلاَّ الله والذِّئْبَ عَلَى غنَمِهِ ، ولكِنَّكُمْ تَسْتَعْجِلُونَ »    رواه البخاري
وفي رواية : « وهُوَ مُتَوسِّدٌ بُرْدةً وقَدْ لقِينَا مِنَ الْمُشْركِين شِدَّةً


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى





Kutoka kwa Abuu Abdillaah, Khabbaab bin Al-Arrat Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Tulimlalamika Mtume naye alikuwa ameegemea shuka yake katika kivuli cha Al-Ka’abah. Tukamwambia: “Hutuombei nusra, hutuombei dua ?” Akatuambia: [Walikuwa waliopita kabla yenu, mtu alikuwa akifukuliwa ardhi na akitiwa humo, halafu ukiletwa msumeno ukiwekwa juu ya kichwa chake, akigawanywa pande mbili, na (mwengine) akichanwa kwa chanuo la chuma akitolewa nyama na mifupa, jambo hilo haliwi kipingamizi katika dini yake. Wa-Allaahi, Mwenyezi Mungu Atalikamilisha jambo hili hata msafiri atembee kutoka San’aa hadi Hadhwramawt hana anachoogopa isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kumkhofia mbwa mwitu asije akala mbuzi wake; lakini ninyi mnaharaka.]    [Imeokewa Bukhari]

Na katika Riwaya nyingine imesema: [Nae alikuwa ameegemea shuka yake. Kwa hakika tulipata mateso makubwa kutoka kwa mushirikina.]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.