SOMO LA MIRATHI
Kama tulivyo elezea sababu na mashari ya mtu kuweza kurithi,pia kuna vizuwizi vya weza kumzuiya mtu kutorithi na viziwizi hivyo ni kama zifuatavyo:
Kizuwizi cha kwanza: Kutafautiana kwa Dini:
Maana yake ni maiti awe na Dini ambayo ni tafauti na wale wanaostahiki kurithi,na kutafautiana katika Dini ni sababu moja ya kumzuiya Mtu Kurithi ,na inakua kama ifuatavyo :
1. Awe maiti ni muislamu na wanorithi ni wakristo au mayahudi au Dini nyeginezo.Kwa hali hii ndugu zake ambao si waislamu hawatoweza kumrithi, na Wanazioni wamekubaliana juu ya hilo kwa Ujmla. Kwa neno lake Mtume wa Mwenyezimungu ﷺ:
[لا يرث المسلم الكافر ولا يرث الكافر المسلم ] رواه البخاري
[Muislamu Hamrithi kafiri na kafiri hamrithi muislamu.] [Imepokewa na Bukhary .]
2. Awe maiti ni kafiri na wanaorithi ni waislamu ,na kwa hali hii pia Muislamu hamrithi ndugu yake kafiri kwa kauli ya jamhuri ya wanachuoni kwa kutegemea Hadithi iliotangulia,
3. Awe maiti ni kafiri kutoka Mila nyengine na wanaorithi pia ni makafiri kutoka Mila nyengine ,hali hiyo pia hawatoeza kurithiana kwa mujibu wa neno lake Mtume ﷺ aliposema:
[لا يتوارث أهل ملتين شتى] رواه أبوداود والترمذي
[hawarithiani wenye Mila mbili tafauti ]. [Imepokewa na Abuu Daudi na Tirmidhiy].
na wanachuoni wamekhtalifiana juu ya hili kuna wanao sema kuwa makafiri wote ni Mila moja, na kuna wanao sema kuwa Uyahudi ni Mila na Ukiristo ni Mila nyingine.
Kizuwizi cha Pili: Kuuwa
Nao ni mtu kumpelekea kutoka kwa roho ya mwanadamu, na muuwaji hawezi kurithi chochote katika mali ya aliemuwa, lau mototo atamuuwa babake basi mototo yule hawezi kumrithi babake kitu chochote .Kwa neon lake Mtume ﷺ:
[ليس للقاتل شيء وإن لم يكن له وارث فوارثه أقرب الناس إليه ولا يرث القاتل شيئا] رواه أبوداود
[hatopata muuaji mali ya mirathi (aliemuwa) na ikiwa hakuna anaemrithi hurithiwa na jamii zake wa karibu na wala harithi muuaji kitu chochote ] [Imepokewa na Daud.]
Na kuuwa kuna hali tofauti kuna mtu kukusudia kuuwa,au kwa bahati mbaya,au kunaofanana na kusudi.Na kuna baadhi ya hali ya mauwaji wanachuoni wameikhatalifiana.
Kizuwizi cha tatu: Utumwa.
Mtumwa harithi wala harithiwi ,na iwapo amerithi basi vyote vinakua ni milki ya Bwana wake.
Na Mwenyezi Mungu mtukufu ameeleze unyonge na kutokuwa na uwezo wa mtume pale aliposema:
{ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا عَبْدًا مَمْلُوكًا لَا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ} النحل:75
[Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiyeweza kitu,] [Al Nahl:75]