0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MASHARTI YA KURITHI

SOMO LA MIRATHI

Sharuti za kurithi ni kama zifuatazo :

Sharti ya Kwanza:

Kua na uhakika wa kifo cha mwenye kurithiwa (mwenye mali)

Na maana ya hayo awe mwenye kurithiwa amekufa, kwa sababu mtu hawezi kurithiwa akiwa hai.

Sampuli za kifo :

A. Uhakika wa kifo, ima kwa kuona au kushuhudia watu waadilifu.

B. Kuhukumiwa nao ni ahukumu kadhi kwa hali ya mtu aliopotea.

Sharti ya Pili:

Uhai wa wenye kurithi:

Maana yake wanaostahiki kurithi wawe hai au walikua hai wakati wa kifo cha marehemu.

Na uhai unakua kwa hali mbili.

1. Uhakika wa uhai ima kwa kuona au kushuhudia na watu waadilifu .

2. Kukadriwa kama vile mtoto akiwa katika tumbo la mamake.
Na ikiwa imetokea ajali na isijulikane nani kamtangulia mwenzake basi hapo
hakuna kurithiana.

Sharti ya tatu:

Kusipatikane ndani yake sababu za kumzuia Mtu kurithi.

Yakipatikan masharti haya pamoja na Sababu za kurithi basi atakuwa na haki mwenyr kurithi kupata fungu lake katika mali ya marehemu.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.