0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

425. Riyadhu Swalihina Mlango Wa Kutaraji (Rehema Za Mwenyezi Mungu.)

باب الرجاء


وعن عبد الله بن عمرو بن العاص – رضي الله عنهما -: أنَّ النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم – تَلاَ قَولَ الله – عز وجل – في إبراهيم – صلى الله عليه وسلم -: ﴿رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضْلَلْنَ كَثِيراً مِنَ النَّاسِ فَمَنْ تَبِعَنِي فَإِنَّهُ مِنِّي﴾ [ إبراهيم: 36 ] الآية، وقَولَ عِيسَى – صلى الله عليه وسلم -: ﴿إِنْ تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ وَإِنْ تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴾ [ المائدة: 118 ] فَرَفَعَ يَدَيهِ وَقالَ: {اللَّهُمَّ أُمّتي أُمّتي} وبَكَى، فَقَالَ الله – عز وجل -: {يَا جِبْريلُ، اذْهَبْ إِلَى مُحَمَّدٍ -وَرَبُّكَ أعْلَمُ – فَسَلْهُ مَا يُبْكِيهِ؟} فَأتَاهُ جبريلُ، فَأخْبَرَهُ رسولُ الله – صلى الله عليه وسلم -، بِمَا قَالَ – وَهُوَ أعْلَمُ – فَقَالَ اللهُ تَعَالَى: {يَا جِبريلُ، اذْهَبْ إِلَى مُحَمّدٍ، فَقُلْ: إنَّا سَنُرْضِيكَ في أُمّتِكَ وَلاَ نَسُوءكَ}    رواه مسلم.


شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى



Imepokewa kutoka kwa Abdullâh bin ‘Amri bin al-‘Âs (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesimulia: “Mtume aliisoma Aya hii katika Sûratu Ibrâhîm: [ Mola wangu! Hakika (masanamu) haya yamepoteza watu wengi. Basi alienifuata ni wangu mimi…] [14:36]. Na akasoma kauli ya Nabii ‘Isa: [ Ikiwa Utawaadhibu, basi bila shaka hao ni waja Wako; na Ukiwasamehe basi kwa hakika Wewe Ndiwe Mwenye Nguvu (na) Mwenye Hikima.] [5:118]. Akainua mikono yake akaomba: “Ewe Mola, umati wangu, umati wangu!” Akalia. Allâh Akasema: “Ee Jibrîl, nenda kwa Muhammad” na Mola wako Anajua zaidi – “kamwulize ni jambo gani likulizalo?” Jibrîl akamwendea, Mtume akamweleza aliyosema, Naye (Allâh) Anajua zaidi. Allâh Akamwambia: “Ewe Jibrîl, nenda kwa Muhammad na umwambie: “Sisi Tutakuridhisha katika umati wako wala Hatutakuonesha vibaya.”   [ Imepokewa na Muslim ]


Begin typing your search above and press return to search.