باب فضل الحب في الله والحث عَلَيهِ وإعلام الرجل من يحبه، أنه يحبه، وماذا يقول لَهُ إِذَا أعلمه
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، عن النَّبيّ – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: {سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمُ اللهُ في ظِلِّهِ يَوْمَ لاَ ظِلَّ إلاَّ ظِلُّهُ: إمَامٌ عَادِلٌ، وَشَابٌّ نَشَأ في عِبَادَةِ الله – عز وجل -، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ بِالمَسَاجِدِ، وَرَجُلاَنِ تَحَابّا في اللهِ اجْتَمَعَا عَلَيهِ وتَفَرَّقَا عَلَيهِ، وَرَجُلٌ دَعَتْهُ امْرَأةٌ ذَاتُ حُسْنٍ وَجَمَالٍ، فَقَالَ: إنِّي أخَافُ الله، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ، فَأخْفَاهَا حَتَّى لاَ تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ الله خَالِياً فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Abû Huraira Radhi za Allah ziwe ju yake amesimulia: “Mtume ﷺ amesema: “Watu saba, Allâh Atawafunika katika kivuli Chake siku ambayo hakutakuwa na kivuli ispokuwa kivuli Chake: kiongozi mwadilifu, kijana aliekulia katika kumwabudu Allâh Aliyeshinda na Kutukuka, mtu ambaye moyo wake umefungamana na Misikiti, watu wawili waliopendana kwa ajili ya Allâh waliojumuika kwa ajili Yake na wakafarikiana kwa ajili Yake, mtu aliyeitwa na mwanamke mwenye sharafu (cheo) na uzuri, akamwambia: Mimi namuogopa Allâh, mtu alietoa sadaka kwa kuficha hata mkono wake wa kushoto usijue kilichotoa mkono wake wa kulia na mtu aliemtaja Allâh faraghani macho yake yakabubujikwa machozi.” [ Wameafikiana na Bukhari na Muslim]