0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

273 Riyadhu Swalihina Mlango wa Kuwafanyia wema Wanawake

BUSTANI YA WATU WEMA

وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: {اسْتَوْصُوا بالنِّساءِ خَيْراً؛ فَإِنَّ المَرْأَةَ خُلِقَتْ مِنْ ضِلعٍ، وَإنَّ أعْوَجَ مَا في الضِّلَعِ أعْلاهُ، فَإنْ ذَهَبتَ تُقيمُهُ كَسَرْتَهُ، وَإنْ تَرَكْتَهُ، لَمْ يَزَلْ أعْوجَ، فَاسْتَوصُوا بالنِّساءِ}      مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية في الصحيحين: {المَرأةُ كالضِّلَعِ إنْ أقَمْتَهَا كَسَرْتَهَا، وَإن اسْتَمتَعْتَ بِهَا، اسْتَمتَعْتَ وفِيهَا عوَجٌ}

وفي رواية لمسلم: {إنَّ المَرأةَ خُلِقَت مِنْ ضِلَع، لَنْ تَسْتَقِيمَ لَكَ عَلَى طَريقة، فإن اسْتَمْتَعْتَ بِهَا اسْتَمْتَعْتَ بِهَا وَفيهَا عوَجٌ، وإنْ ذَهَبْتَ تُقِيمُهَا كَسَرْتَها، وَكَسْرُهَا طَلاَقُهَا}


Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amepokea kutoka kwa Mtume Amesema [Wafanyieni kheri wanawake, hakika mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na hakika sehemu iliopotoka zaidi katika ubavu ni ile ya juu, ukitaka kuunyosha utauvunja, na ukiuvunja utaendela kupotoka; kwa hivyo wafanyieni wema wanawake]     [Wameafikiana Bukhari na Muslim]

Na katika riwaya ilio katika sahihi mbili (Bukhari na Muslim : [Mwanamke ni kama ubavu, ukitaka kuunyosha utauvunja, na ukistarehe naye utastarehe naye akiwa amepotoka]

Na katika Riwaya ya Muslim: [Hakika mwanamke ameumbwa kwa ubavu hatakunyokea katika njia, ukistarehe naye utastarehe naye akiwa amepotoka, na ukitaka kuunyosha utauvunja, na kuuvunja kwake ni talaka.]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.