BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي هريرة – رضي الله عنه -، قَالَ: قَالَ رَسُول الله – صلى الله عليه وسلم -، قَالَ: {اسْتَوْصُوا بالنِّساءِ خَيْراً؛ فَإِنَّ المَرْأَةَ خُلِقَتْ مِنْ ضِلعٍ، وَإنَّ أعْوَجَ مَا في الضِّلَعِ أعْلاهُ، فَإنْ ذَهَبتَ تُقيمُهُ كَسَرْتَهُ، وَإنْ تَرَكْتَهُ، لَمْ يَزَلْ أعْوجَ، فَاسْتَوصُوا بالنِّساءِ} مُتَّفَقٌ عَلَيهِ
وفي رواية في الصحيحين: {المَرأةُ كالضِّلَعِ إنْ أقَمْتَهَا كَسَرْتَهَا، وَإن اسْتَمتَعْتَ بِهَا، اسْتَمتَعْتَ وفِيهَا عوَجٌ}
وفي رواية لمسلم: {إنَّ المَرأةَ خُلِقَت مِنْ ضِلَع، لَنْ تَسْتَقِيمَ لَكَ عَلَى طَريقة، فإن اسْتَمْتَعْتَ بِهَا اسْتَمْتَعْتَ بِهَا وَفيهَا عوَجٌ، وإنْ ذَهَبْتَ تُقِيمُهَا كَسَرْتَها، وَكَسْرُهَا طَلاَقُهَا}
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake amepokea kutoka kwa Mtume Amesema [Wafanyieni kheri wanawake, hakika mwanamke ameumbwa kwa ubavu, na hakika sehemu iliopotoka zaidi katika ubavu ni ile ya juu, ukitaka kuunyosha utauvunja, na ukiuvunja utaendela kupotoka; kwa hivyo wafanyieni wema wanawake] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]
Na katika riwaya ilio katika sahihi mbili (Bukhari na Muslim : [Mwanamke ni kama ubavu, ukitaka kuunyosha utauvunja, na ukistarehe naye utastarehe naye akiwa amepotoka]
Na katika Riwaya ya Muslim: [Hakika mwanamke ameumbwa kwa ubavu hatakunyokea katika njia, ukistarehe naye utastarehe naye akiwa amepotoka, na ukitaka kuunyosha utauvunja, na kuuvunja kwake ni talaka.]