BUSTANI YA WATU WEMA
عن سعد بن أَبي وَقَّاص رضي اللَّه عنه قال : كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم سِتَّةَ نفَر ، فقال المُشْرِكُونَ للنَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : اطْرُدْ هُؤُلاءِ لا يَجْتَرِئُون عليْنا ، وكُنْتُ أَنا وابْنُ مسْعُودٍ ورجُل مِنْ هُذَيْلِ وبِلال ورجلانِ لَستُ أُسمِّيهِما ، فَوقَعَ في نَفْسِ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ما شاءَ اللَّه أَن يقعَ فحدث نفْسهُ ، فأَنْزَلَ اللَّهُ تعالى : { ولا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُون رَبَّهُمْ بالْغَداةِ والعَشِيِّ يُريدُونَ وجْهَهُ } [ الأنعام : 52 ] رواه مسلم
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Imepokewa kutoka kwa Sa’d bin Abî Waqqâs Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: “Tulikuwa pamoja na Mtume ﷺ kundi la watu sita. Mushrikina wakamwambia Mtume ﷺ : “Wafukuze hawa (watu sita) wasije wakatufanyia ujasiri.” Na hapo nilikuwa mimi, Ibni Mas‘ûd, mtu mmoja katika kabila la Hudhail, Bilâl na watu wawili ambao sitawataja. Ikaingia katika moyo wa Mtume ﷺ Alichokitaka Allâh kuingia (yaani kuwafukuza), akaizungumza nafsi yake. Allâh Akateremsha: “Wala usiwafukuze wale wanaomwabudu Mola wao asubuhi na jioni kutaka Radhi Yake.” 6:52. [Imepokewa na Muslim.]