BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبي هريرة رضي اللَّه عنه قال : قال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « كُلُّ سُلامى مِنَ النَّاسِ عَلَيْهِ صَدَقَةٌ كُلَّ يوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ : تَعْدِلُ بيْن الاثْنَيْنِ صَدقَةٌ ، وَتُعِينُ الرَّجُلَ فِي دَابَّتِهِ فَتحْمِلُهُ عَلَيْهَا ، أَوْ تَرْفَعُ لَهُ عَلَيْهَا مَتَاعهُ صَدقَةٌ، وَالْكَلِمَةُ الطَّيبةُ صدقَةٌ ، وبكُلِّ خَطْوَةٍ تَمْشِيهَا إِلَى الصَّلاةِ صَدقَةٌ ، وَتُمِيطُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ » متفق عليه
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za Allah ziwe juu yao) amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ : [Viungo vyote vya wanadamu vinawajibika kutoa Sadaka kwa kila siku inayochomozewa na Jua: Kusuluhisha kwa uadilifu baina ya watu wawili ni Sadaka, kumsaidia juu ya Mnyama wake ukampandisha au ukamnyanyulia Mzogo wake ni Sadaka, kusema neno zuri ni Sadaka, kila hatua unayopiga kwenda Msikitini ni Sadaka, na kuondoa taka njiani ni Sadaka] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله