BUSTANI YA WATU WEMA
عن ابن مَسْعُودٍ رضي اللَّه عنه قال : قال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : «إِنَّ أَوَّلَ مَا دخَلَ النَّقْصُ عَلَى بَنِي إِسْرائيلَ أَنَّه كَانَ الرَّجُلُ يَلْقَى الرَّجُلَ فَيَقُولُ : يَا هَذَا اتَّق اللَّه وَدعْ مَا تَصْنَعُ فَإِنَّهُ لا يَحِلُّ لك ، ثُم يَلْقَاهُ مِن الْغَدِ وَهُو عَلَى حالِهِ ، فلا يمْنَعُه ذلِك أَنْ يكُونَ أَكِيلَهُ وشَرِيبَهُ وَقعِيدَهُ ، فَلَمَّا فَعَلُوا ذَلِكَ ضَرَبَ اللَّه قُلُوبَ بَعْضِهِمْ بِبَعْضٍ » ثُمَّ قال : { لُعِنَ الَّذِينَ كَفَروا مِنْ بنِي إِسْرَائِيلَ عَلَى لِسَانِ داوُدَ وعِيسَى ابنِ مَرْيمِ ذلِك بما عَصَوْا وكَانوا يعْتَدُونَ ، كَانُوا لا يَتَنَاهَوْنَ عنْ مُنْكَرٍ فَعَلُوهُ لَبِئْسَ ما كانُوا يَفْعلُون تَرى كثِيراً مِنْهُمُ يَتَوَلَّوْنَ الَّذينَ كَفَرُوا لَبِئْسَ مَا قَدَّمتْ لَهُمْ أَنْفُسُهُمْ
إلى قوله : { فَاسِقُونَ } [ المائدة : 78، 81 } ثُمَّ قَالَ : « كَلاَّ ، وَاللَّه لَتَأْمُرُنَّ بالْمعْرُوفِ ، وَلَتَنْهوُنَّ عَنِ الْمُنْكَرِ، ولَتَأْخُذُنَّ عَلَى يَدِ الظَّالِمِ ، ولَتَأْطِرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ أَطْراً ، ولَتقْصُرُنَّهُ عَلَى الْحَقِّ قَصْراً ، أَوْ لَيَضْرِبَنَّ اللَّه بقُلُوبِ بَعْضِكُمْ عَلَى بَعْضٍ ، ثُمَّ لَيَلْعَنكُمْ كَمَا لَعَنَهُمْ » رواه أبو داود، والترمذي وقال : حديث حسن
Kutoka kwa Ibn Mas’uwd Radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume ﷺ amesema: “Upungufu wa kwanza uliowafikia Banuu Israiyl ulikuwa mtu kukutana na mwenzake, akimwambia: Ewe fulani! muogope Mwenyezi Mungu na uache unayofanya kwani si halali kwako (kufanya hivyo). Kisha anakutana naye siku ya pili katika hali yake ile ile (bila ya mabadiliko), hilo halimkatazi yeye kutokula naye, kunywa na kukaa naye. Walipofanya hivyo, Mwenyezi Mungu Alibadilisha mioyo yao baadhi yao kwa wengine.” Kisha akasoma: [Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka.Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya!Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na walio kufuru. Hakika ni maovu yaliyo tangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia, nao watadumu katika adhabu.Na lau wangeli kuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu, na huyu Nabii, na yaliyo teremshwa kwake, wasingeli wafanya hao marafiki. Lakini wengi katika wao ni wapotofu.] [Al-Maaida: 78-81]
Kisha akasema: [Hasha! Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu ya kwamba mutaendelea kuamrishana mema na kukataza maovu na kuushika mkono wa dhalimu na kuwashawishi wafanye uadilifu, kuwafanya wawe imara juu ya haki na ukweli. Mkishindwa kufanya hivyo, basi jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu Atawagongesha nyo zenu baadhi yenu kwa wengine (mutachukiana na kufarikiana) na kisha Atawalaani kama Alivyowalaani wao (Mayahudi).] [Imepokewa na Abuu Daud na AtTirmidhi na amesema Hadithi hii ni Hassan]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله