BUSTANI YA WATU WEMA
عَنْ أَبِي سعيدٍ الْحسنِ البصْرِي أَنَّ عَائِذَ بن عمْروٍ رضي اللَّه عنه دخَلَ عَلَى عُبَيْدِ اللَّهِ بن زيَادٍ فَقَالَ : أَيْ بن زيَادٍ فَقَالَ : أَيْ بنيَّ ، إِنِّي سمِعتُ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يَقولُ : « إِنَّ شَرَّ الرِّعاءِ الْحُطَمَةُ » فَإِيَّاكَ أَنْ تَكُونَ مِنْهُمْ . فَقَالَ لَهُ : اجْلِسْ فَإِنَّمَا أَنت مِنْ نُخَالَةِ أَصْحَابِ مُحَمَّدٍ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، فقال : وهَلْ كَانَتْ لَهُمْ نُخَالَةٌ إِنَّمَا كَانَتِ النُّخالَةُ بَعْدَهُمْ وَفي غَيرِهِمْ ، رواه مسلم
Kutoka kwa Abu Sa’iid Al-Hasan Al-Baswariy ya kwamba: ‘Aa’idh bin ‘Amru Radhi za Allah ziwe juu yake alimtembelea Ubaydullaah bin Ziyaad (Alikuwa ni Gavana wa Yaziid katika nchi ya Iraq) kumwambia: Ewe mtoto wangu! hakika nimesikia Mtume ﷺ akisema: [Hakika mchungaji mbaya kabisa ni wenye moyo mgumu] (anaedhulumu watu). Basi nakutahadharisha usiwe miongoni mwao.” (Abdullah bin Zayd) akamwambia Keti kwani wewe ni miongoni mwa baki ya Maswahaba wa Muhammad ﷺ. (yaani si mtu wa Maana) Akasema: (‘Aa’idh) na je, yeye alikuwa na mabaki? hakika mabaki ni waliokuja baada yao na wengineo. [Imepokewa na Muslim]
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله