BUSTANI YA WATU WEMA
وعن أَبِي هريرة رضي اللَّه عنه أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : «منْ دَعَا إِلَى هُدًى كَانَ لَهُ مِنَ الأَجْرِ مِثْلُ أُجُورِ منْ تَبِعَهُ لا ينْقُصُ ذلِكَ مِنْ أُجُورِهِم شَيْئاً ، ومَنْ دَعَا إِلَى ضَلاَلَةٍ كَانَ عَلَيْهِ مِنَ الإِثْمِ مِثْلُ آثَامِ مَنْ تَبِعَهُ لا ينقُصُ ذلكَ مِنْ آثَامِهِمْ شَيْئاً » رواه مسلم
Kutoka kwa Abuu Hurayrah Radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ amesema: [Mwenye kulingania (watu) katika uongofu atapata thawabu mfano wa wale wenye kumfuata wala hilo haliwapunguzii thawabu zao hata kidogo. Na yeyote atakayewaita watu katika upotevu atapata madhambi mfano wa madhambi ya wale wenye kumfuata na wala hilo halitawapunguzia madhambi hata chembe.] [Imepokewa na Muslim]