BUSTANI YA WATU WEMA
عَنْ أَبِي سعيدٍ عبدِ اللَّهِ بنِ مُغَفَّلٍ ، رضي اللَّه عنه ، قال : نَهَى رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، عَن الخَذْفِ وقالَ : « إِنَّهُ لا يقْتُلُ الصَّيْدَ ، ولا يَنْكَأُ الْعَدُوَّ ، وَإِنَّهُ يَفْقَأُ الْعَيْنَ ، ويَكْسِرُ السِّنَّ » متفقٌ عليه
وفي رواية : أَنَّ قريباً لابْنِ مُغَفَّلٍ خَذَفَ ، فَنَهَاهُ وقال : إِنَّ رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم نَهَى عن الخَذْفِ وقَالَ : « إِنَّهَا لا تَصِيدُ صَيْداً » ثُمَّ عادَ فقالَ : أُحَدِّثُكَ أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم ، نَهَى عَنْهُ ، ثُمَّ عُدْتَ تَخْذِفُ ،؟ لا أُكَلِّمُكَ أَبداً
Kutoka kwa Abuu Sa’yd, ‘Abdullaah bin Mughaffal Radhi za Allah ziwe juu yake Amesea Mtume ﷺ amekataza al-khadhaf’ (kurusha vijiwe kwa kutumia kidole gumba na cha shahaada) akasema: [Kwani hakiuwi windo wala hakimuuwi adui, bali hutoboa jicho na kuvunja jino tu.] [Imepokewa na Bukhaariy na Muslim]
Na katika Riwaya nyingine ya Muslim imesema:
“Jamaa mmoja wa karibu kwa Ibn Mughaffal alifanya khadhaf. Akamkataza na akamwambia: Mtume ﷺ amekataza kitendo hiki (khadhaf), akasema: [Kwani hakiwindi windo] Kisha yule jamaa akarudia kitendo hicho. Akamwambia: Nimekuhadithia kuwa Mtume ﷺ amekataza jambo hilo kisha umerudia kitendo hicho cha khadhaf? Sitazungumza nawe kamwe!] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]