0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

150. Riyadhu Swalihina Mlango wa kufanya Ibada kwa kiasi Hadithi ya 09


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن أَبِي محمد عبدِ اللَّهِ بن عمرو بنِ العاص رضي اللَّه عنهما قال : أُخْبرَ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أنِّي أَقُول : وَاللَّهِ لأَصومَنَّ النَّهَارَ ، ولأَقُومنَّ اللَّيْلَ ما عشْتُ ، فَقَالَ رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : «أَنْتَ الَّذِي تَقُول ذلك ؟»  فَقُلْت له : قَدْ قُلتُه بأَبِي أَنْتَ وأُمِّي يا رسولَ اللَّه . قَالَ: « فَإِنكَ لا تَسْتَطِيعُ ذلِكَ ، فَصُمْ وأَفْطرْ ، ونَمْ وَقُمْ ، وَصُمْ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ فَإِنَّ الْحسنَةَ بعَشْرِ أَمْثَالهَا ، وذلكَ مثْلُ صِيامٍ الدَّهْرِ»  قُلْت : فَإِنِّي أُطيق أفْضَلَ منْ ذلكَ قالَ : « فَصمْ يَوْماً وَأَفْطرْ يَوْمَيْنِ ،» قُلْت : فَإِنِّي أُطُيق أفْضَلَ مِنْ ذلكَ ، قَالَ : « فَصُم يَوْماً وَأَفْطرْ يوْماً ، فَذلكَ صِيَام دَاوود صلى الله عليه وسلم، وَهُو أَعْدَل الصِّيَامِ » . وَفي رواية : « هوَ أَفْضَلُ الصِّيامِ » فَقُلْتُ فَإِنِّي أُطِيقُ أَفْضَلَ مِنْ ذلكَ ، فقال رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « لا أَفْضَلَ منْ ذلك» وَلأنْ أَكْونَ قَبلْتُ الثَّلاثَةَ الأَيَّامِ الَّتِي قال رسولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَحَبُّ إِليَّ منْ أَهْلِي وَمَالِى
وفي روايةٍ : « أَلَمْ أُخْبَرْ أَنَّكَ تَصومُ النَّهَارَ وتَقُومُ اللَّيْلَ ؟ » قلت : بلَى يَا رسول اللَّهِ . قال : « فَلا تَفْعل : صُمْ وأَفْطرْ ، ونَمْ وقُمْ فَإِنَّ لجَسَدكَ علَيْكَ حقًّا ، وإِنَّ لعيْنَيْكَ عَلَيْكَ حَقًّا وَإِنَّ لزَوْجِكَ علَيْكَ حَقًّا ، وَإِنَّ لزَوْركَ عَلَيْكَ حَقًّا ، وإِنَّ بحَسْبكَ أَنْ تَصْومَ فِي كُلِّ شَهْرٍ ثَلاثَةَ أَيَّامٍ ، فَإِنَّ لَكَ بِكُلِّ حَسَنةٍ عشْرَ أَمْثَالِهَا ، فَإِذن ذلك صِيَامُ الدَّهْرِ» فشَدَّدْتُ فَشُدِّدَ عَلَيَّ ، قُلْتُ : يا رسول اللَّه إِنّي أَجِدُ قُوَّةً، قال : « صُمْ صِيَامَ نَبِيِّ اللَّهِ داوُدَ وَلا تَزدْ عَلَيْهِ» قلت: وما كَان صِيَامُ داودَ؟ قال : « نِصْفُ الدهْرِ » فَكَان عَبْدُ اللَّهِ يقول بعْد مَا كَبِر : يالَيْتَنِي قَبِلْتُ رُخْصةَ رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم
وفي رواية : « أَلَمْ أُخْبَرْ أَنَّك تصُومُ الدَّهْرِ ، وَتْقَرَأُ الْقُرْآنَ كُلَّ لَيْلَة ؟ » فَقُلْتُ : بَلَى يا رسولَ اللَّهِ ، ولَمْ أُرِدْ بذلِكَ إِلاَّ الْخيْرَ ، قَالَ : « فَصُمْ صَوْمَ نَبِيِّ اللَّهِ داودَ ، فَإِنَّه كَانَ أَعْبَدَ النَّاسِ ، واقْرأْ الْقُرْآنَ في كُلِّ شَهْرٍ » قُلْت : يَا نَبِيِّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيق أَفْضل مِنْ ذلِكَ ؟ قَالَ : « فَاقْرَأه فِي كُلِّ عِشرِينَ » قُلْت : يَا نبيِّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيق أَفْضَل مِنْ ذَلِكَ ؟ قَالَ : «فَاقْرَأْهُ فِي كُلِّ عَشْر » قُلْت : يَا نَبِيَّ اللَّهِ إِنِّي أُطِيق أَفْضلَ مِنْ ذلِكَ ؟ قَالَ  « فَاقْرَأْه في كُلِّ سَبْعٍ وَلاَ تَزِدْ عَلَى ذَلِكَ » فَشَدَّدْتُ فَشُدِّدَ عَلَيَّ ، وقَالَ لِي النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « إِنَّكَ لاَ تَدْرِي لَعلَّكَ يَطُول بِكَ عُمُرٌ قالَ : فَصِرْت إِلَى الَّذِي قَالَ لِي النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَلَمَّا كَبِرْتُ وَدِدْتُ أنِّي قَبِلْت رخْصَةَ نَبِيِّ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم
وفي رواية : « وَإِنَّ لوَلَدِكَ علَيْكَ حَقًّا » وفي روايةٍ : « لا صَامَ من صَامَ الأَبَدَ » ثَلاثاً . وفي روايةٍ : « أَحَبُّ الصَّيَامِ إِلَى اللَّه تَعَالَى صِيَامُ دَاوُدَ ، وَأَحَبُّ الصَّلاةِ إِلَى اللَّهِ تَعَالَى صَلاةُ دَاوُدَ : كَانَ يَنَامُ نِصْفَ اللَّيلِ ، وَيَقُومُ ثُلُثَهُ ، وَيَنَامُ سُدُسَهُ ، وَكَانَ يَصُومُ يوْماً ويُفْطِرُ يَوْماً ، وَلا يَفِرُّ إِذَا لاقَى
وفي رواية قَالَ : أَنْكَحَنِي أَبِي امْرَأَةً ذَاتَ حسَبٍ ، وكَانَ يَتَعَاهَدُ كَنَّتهُ أي : امْرَأَة ولَدِهِ فَيسْأَلُهَا عَنْ بَعْلِهَا ، فَتَقُولُ لَهُ : نِعْمَ الرَّجْلُ مِنْ رجُل لَمْ يَطَأْ لنَا فِرَاشاً ولَمْ يُفتِّشْ لنَا كَنَفاً مُنْذُ أَتَيْنَاهُ فَلَمَّا طالَ ذَلِكَ عليه ذكَرَ ذلِكَ لِلنَّبِيِّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم . فقَالَ : « الْقَني به » فلَقيتُهُ بَعْدَ ذلكَ فَقَالَ  « كيفَ تَصُومُ ؟ » قُلْتُ كُلَّ يَوْم ، قَالَ : « وَكيْفَ تَخْتِم ؟ » قلتُ: كُلَّ لَيلة ، وذَكَر نَحْوَ مَا سَبَق وكَان يقْرَأُ عَلَى بعْض أَهْلِه السُّبُعَ الَّذِي يقْرؤهُ ، يعْرضُهُ مِن النَّهَارِ لِيكُون أَخفَّ علَيِهِ بِاللَّيْل ، وَإِذَا أَراد أَنْ يَتَقَوَّى أَفْطَر أَيَّاماً وَأَحصَى وصَام مِثْلَهُنَّ كَراهِيةَ أَن يتْرُك شيئاً فارقَ علَيهِ النَّبِي صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم
كُلُّ هذِه الرِّوَايات صحيِحةٌ مُعْظَمُهَا فِي الصَّحيحيْنَ وقليلٌ منْهَا في أَحَدِهِما


Kutoka kwa Abuu Muhammad, ‘Abdillaah bin ‘Amruw bin Al-‘Aasw Radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Mtume ﷺ aliaambiwa kuwa mimi nasema: Wa-Allaahi nitafunga mchana na nitaswali usiku maisha yangu yote. Mtume ﷺ akaniuliza: [Wewe ndiye uliyesema hivyo?] Nikamjibu: Ndiyo, hakika nimesema, nakutolee fidia baba yangu na mama yangu Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akaniambia: [Wewe hutaweza kufanya hivyo, basi funga na ule, lala (usiku) na uswali, na ufunge siku tatu kila mwezi; kwani jema moja hulipwa kwa mema kumi mfano wake, na hiyo ni kama saumu  ya Mwaka (mzima)!] Nikamwambia: Mimi naweza kufanya zaidi ya hivyo. Akaniambia: [Basi funga siku moja na ule siku mbili.] Nikamwambia: Mimi naweza zaidi ya hivyo. Akanambia: [Basi funga siku moja na ule siku moja, na hiyo ndio Funga ya Nabii Daawuwd (‘Alayhis Salaam) nayo ndio Funga ya wastani zaidi.]

Na katika Riwaya nyingine imesema: [Hiyo ndiyo Funga bora zaidi.] Nikamwambia: Mimi naweza zaidi ya hivyo. Mtume akaniambia: [Hakuna bora zaidi ya hivyo.] Kwa kweli lau ningelikubali zile siku tatu alizonipa Mtume ﷺ ingelipendeza kwangu zaidi kulikoni familia yangu na mali yangu.

Na katika Riwaya nyingine imesema: [Si niliambiwa kuwa wewe unafunga mchana na unaswali usiku wote ?] Nikamjibu: Ndiyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akaniambia: [Usifanye hivyo, funga na ule, lala na uswali, hakika mwili wako una haki juu yako, na macho yako yana haki juu yako, na mkeo ana haki juu yako na mgeni wako ana haki juu yako, na hakika inakutosha ufunge siku tatu kila mwezi; kwani katika kila jambo jema moja unapata mema kumi mfano wake; huko ndiyo Funga ya Mwaka (mzima)!] Nikamkazania, nami nikakaziwa. Nikamwambia: Mtume wa Mwenyezi Mungu, nina nguvu zaidi. Akanambia: [Funga Saumu ya Nabii Daawuwd wala usizidishe juu ya hapo.] Nikamuuliza: Saumu ya Nabii Daawuwd ilikuwaje? Akaniambia: [Nusu ya Mwaka.]

‘Abdullaah alipozeeka alikuwa akisema: Laiti kama ningelikubali ruhusa ya Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ.

Na katika Riwaya nyingine imesema: [Si niliambiwa kuwa unafunga Saumu ya Mwka na unasoma Qur’ani yote kila usiku?] Nikamjibu: Ndiyo Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala sijakusudia kufanya hivyo ila ni kheri tu. Akaniambia: [Funga Saumu ya Nabii Daawuwd; kwani yeye aliwashinda watu kwa ‘ibaada, na soma (ukhitimishe) Qur’ani kila mwezi.] Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza zaidi ya hivyo. Akaniambia: [Soma kwa siku ishirini.] Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza zaidi ya hivyo. Akaniambia: [Soma kwa siku kumi.] Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza zaidi ya hivyo. Akaniambia: [Soma umalize kila baada ya siku saba, wala usizidishe uchache wa hapo.] Nikatia mkazo nami nikakaziwa. Mtume akaniambia: [Huwezi kujua pengine unaweza kuwa na umri mrefu.] Na kweli nikawa kama alivyoniambia Mtume .

Na katika Riwaya nyingine imesema: [Na hakika mwanao ana haki juu yako.]

Na Riwayah nyengine: [Hana Funga mwenye kufunga daima.] Alikariri mara tatu.

Na Riwaya nyingine imesema: [Saumu ipendezayo zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Saumu ya Nabii Daawuwd. Na Swalaa ipendezayo zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni Swala ya Nabii Daawuwd; alikuwa akilala nusu ya usiku, akiswali thuluthi yake, akilala sudusi yake, na alikuwa akifunga siku moja na akila siku moja, wala hakimbii anapokutana na adaui (vitani).]

Na Riwaya nyingine imesema: Baba yangu alinioza mke mwenye nasaba nzuri, na alikuwa akimjulia hali mkwewe, akamuuliza hali ya mumewe, naye akimwambia: Mtu mzuri miongoni mwa watu. Kuanzia anioe, hakuja kulala na mimi wala kujamiiana nami. Hali hii ilipoendelea kwa muda mrefu, alitajiwa Mtume . Akasema: [Nileteeni kwangu]. Nami nikamuendea. Akaniuliza: [Unafunga vipi?] Nikamjibu: Kila siku. Akaniuliza: [Unahitimisha vipi Qur’ani?] Nikamjibu: Kila usiku. Akataja Hadithi ambayo imetangulia kuelezwa.

‘Abdullaah alikuwa akisoma kwa baadhi ya familia yake subu’ anayoisoma (yaani alikuwa akihitimisha kwa siku saba), akiisoma mchana ili apate tahfifu wakati wa usiku. Na anapotaka tahfifu kwa kufunga kila siku alikuwa anaacha kufunga baadhi ya siku na baadaye kuzilipa. Anafanya hivyo kwa kuchelea asije kuacha mazoea aliyokuwaw akati Mtume  anafariki.

Na Riwaya zote ni Sahihi nyingi zake ziko katika Sahihi mbili na nichache zilioko katika moja kati ya sahihi mbili.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.