0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

149. Riyadhu Swalihina Mlango wa kufanya Ibada kwa kiasi Hadithi ya 08


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


وعن أَبِي جُحَيْفَةَ وَهبِ بْنِ عبد اللَّه رضي اللَّهُ عنه قال : آخَى النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم بَيْن سَلْمَانَ وأَبِي الدَّرْدَاءِ ، فَزَارَ سلْمَانُ أَبَا الدَّرْدَاءِ ، فَرَأَى أُمَّ الدَّرْدَاء مُتَبَذِّلَةً فقالَ : ما شَأْنُكِ؟ قالَتْ : أَخْوكَ أَبُو الدَّرداءِ ليْسَ له حَاجةٌ فِي الدُّنْيَا . فَجَاءَ أَبُو الدرْدَاءِ فَصَنَعَ لَه طَعَاماً ، فقالَ لَهُ : كُلْ فَإِنِّي صَائِمٌ ، قالَ : ما أَنا بآكلٍ حَتَّى تأْكلَ ، فَأَكَلَ ، فَلَّمَا كانَ اللَّيْلُ ذَهَبَ أَبُو الدَّرْداءِ يقُوم فقال لَه : نَمْ فَنَام ، ثُمَّ ذَهَبَ يَقُوم فقالَ لَه : نَمْ ، فَلَمَّا كان من آخرِ اللَّيْلِ قالَ سلْمانُ : قُم الآنَ، فَصَلَّيَا جَمِيعاً ، فقالَ له سَلْمَانُ : إِنَّ لرَبِّكَ عَلَيْكَ حَقًّا ، وَإِنَّ لنَفْسِكَ عَلَيْكَ حقًّا ، ولأهلِك عَلَيْكَ حَقًّا ، فَأَعْطِ كُلَّ ذِي حَقٍّ حَقَّه ، فَأَتَى النَّبِيَّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم فَذَكر ذلكَ لَه ، فقالَ النَّبِيُّ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم : « صَدَقَ سلْمَانُ »            رواه البخاري


Kutoka kwa Abuu Juhayfah, Wahb bin ‘Abdillaah Radhi za Allah ziwe juu amesema: Mtume ﷺ alifunga undugu baina ya Salmaan na Abuu Dar’daa. Salmaan akaenda kumtembelea Abuu Dardaa, akamuona mama Dardaa amevaa nguo iliyochakaa. Akamuuliza: Mbona upo hivyo? Akasema: Nduguyo Abuu Dardaa hana haja ya dunia (hataki wanawake). Abuu Dardaa akaja, akamtengenezea chakula nduguye (Salmaan) kisha akamwambia: Kula mimi nimefunga. Salmaan akamwambia: Sitokula mpaka uanze wewe kula. Akala. Ulipofika usiku Abuu Dardaa akataka kuanza kuswali (Swala ya usiku). Salmaan akamwambia: Lala. Akalala. Ulipofika mwisho wa usiku Salmaan akamwambia sasa amka (uswali). Wakaswali wote. Kisha Salmaan akamwambia: Hakika Mola wako Ana haki juu yako, na nafsi yako ina haki juu yako, na mkeo na familia yako wana haki juu yako. Kwa hiyo kila mmoja mpe haki yake.  Abuu Dardaa akamuendea Mtume  akatajiwa hayo, hapo Mtume ﷺ akasema: [Amekuambia kweli Salmaan]      [Imepokewa na Muslim]


 شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.