BUSTANI YA WATU WEMA
عن أبي هريرة رضي اللَّه عنه أَن رسولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال يوم خيْبر: «لأعطِينَّ هذِهِ الراية رجُلا يُحبُّ اللَّه ورسُوله، يفتَح اللَّه عَلَى يديهِ» قال عمر رضي اللَّهُ عنه: ما أَحببْت الإِمارة إلاَّ يومئذٍ فتساورْتُ لهَا رجَاءَ أَنْ أُدْعى لهَا، فدعا رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم عليَ بن أبي طالب، رضي اللَّه عنه، فأَعْطَاه إِيَّاها، وقالَ: «امش ولا تلْتَفتْ حتَّى يَفتح اللَّه عليكَ» فَسار عليٌّ شيئاً، ثُمَّ وقف ولم يلْتفتْ، فصرخ: يا رسول اللَّه، على ماذَا أُقاتل النَّاس؟ قال: «قاتلْهُمْ حتَّى يشْهدوا أَنْ لا إله إلاَّ اللَّه، وأَنَّ مُحمَّداً رسول اللَّه، فَإِذا فعلوا ذلك فقدْ منعوا منْك دماءَهُمْ وأَموالهُمْ إلاَّ بحَقِّها، وحِسابُهُمْ على اللَّهِ» رواه مسلم
«فَتَساورْت» هو بالسِّين المهملة: أَيْ وثبت مُتطلِّعاً
شرح الحديث مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى
Kutoka kwa Abuu Hurayra Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume ﷺ :Alisema siku ya Vita vya Khaybar: [Kwa hakika nitampa mtu bendera hii anayempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu Ataleta ushindi kwa sababu yake.] ‘Umar Radhi za Allah ziwe juu yake anasema: Sikuwahi kuupenda uongozi isipokuwa siku hiyo. Mtume ﷺ akamuita ‘Ali bin Abiy Twaalib, akampa bendera ile. Akamwambia: [Nenda wala usigeuke mpaka Mwenyezi Mungu Akupe ushindi.” ‘Ali akatembea kidogo. Kisha akasimama wala hakugeuka nyuma, akauliza kwa sauti ya juu: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane na watu juu ya nini? Akamwambia: [Pigana nao mpaka washuhudie kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa wa haki ispokuwa Mwenyezi Mungu, na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wakifanya hivyo, wameshahifadhika kutokana na nawe katika damu zao na mali yao ila kwa haki yake, na hisabu yao ipo kwa Mwenyezi Mungu.] [Imepokewa na Muslim ]