0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

11. MLANGO WA MUJAHADA (KUFANYA JUHUDI)


BUSTANI YA WATU WEMA


1463655589


   قال اللَّه تعالى : {وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ}       العنكبوت:69

 

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na wanao fanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema]     [Suurat Al A’nkabut:29]

 

99:وقال تعالى :{وَاعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ الْيَقِينُ}   الحجر

 

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini.]      [Suuratul Hijr:99]

 

8:وقال تعالى :{وَاذْكُرِ اسْمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلْ إِلَيْهِ تَبْتِيلًا}   المزمل

 

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na lidhukuru jina la Mola wako Mlezi, na ujitolee kwake kwa ukamilifu.]       [Surat Al-Muzzammil:8]

 

20:وقال تعالى :{وَمَا تُقَدِّمُوا لِأَنفُسِكُم مِّنْ خَيْرٍ تَجِدُوهُ عِندَ اللَّهِ هُوَ خَيْرًا وَأَعْظَمَ أَجْرًا ۚ }   المزمل

 

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na kheri yoyote mnayo itanguliza kwa ajili ya nafsi zenu mtaikuta kwa Mwenyezi Mungu, imekuwa bora zaidi, na ina thawabu kubwa sana.]      [Surat Al-Muzzammil:20]

 

215:وقال تعالى :{وَمَا تَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ}   البقرة

 

Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[Na kheri yoyote mnayo ifanya Mwenyezi Mungu anaijua.]       [Sura Al-Baqara:215]

 

والآيات في الباب كثيرة معلومة

Na aya katika Mlango huu ni nyingi zajulikana.


 شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى




Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.