BUSTANI YA WATU WEMA
قال اللَّه تعالى : {فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ} هود:112
وقال تعالى :{إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا تَتَنَزَّلُ عَلَيْهِمُ الْمَلَائِكَةُ أَلَّا تَخَافُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَبْشِرُوا بِالْجَنَّةِ الَّتِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ نَحْنُ أَوْلِيَاؤُكُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَشْتَهِي أَنفُسُكُمْ وَلَكُمْ فِيهَا مَا تَدَّعُونَ نُزُلًا مِّنْ غَفُورٍ رَّحِيمٍ} فصلت:30-32
وقال اللَّه تعالى : {إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ} الأحقاف:13
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Basi, simama sawa sawa kama ulivyo amrishwa,] [Huud:112]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa.Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka.Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.] [Suuratul Fuss’ilat:30-32]
Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:
[Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu; kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu, wala hawatahuzunika.] [Suuratul Al Ah’qaaf:13]
شرح مقدمة الباب مع فضيلة الشيخ خالد بن عثمان السبت حفظه الله تعالى